Katibu
Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar
es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa
kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa
(ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA KAJUNASON BLOG/MMG.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati wa
halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo
wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao
makao makuu jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na
watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam
(Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika
mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika
katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco).
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa na watendaji
wengine wakati wakiimba wimbo wa 'Tanzani', 'Tanzania'.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
amesema ameapa kuwashughulikia watumishi wachache chini ya wizara yake
ambao bado wanaendekeza maisha ya ujanja ujanja kazini.
Profesa Kitila ameitoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na
watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam
(Dawasco) kwenye ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es
Salaam.
Amesema
ingawa Dawasco imefanikiwa kuboresha huduma zake, lakini wapo watumishi
wa chache ambao bado wanafanya kazi kwa ubabaishaji.
Amesisitiza kuwa zama za ujanjaujanja zimekwisha na wale wachache
wanaoshiriki mbinu za kulihujumu shirika hilo hawatavumiliwa na
watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa watakaobainika.
Wakati
huo mhuo, Profesa Mkumbo amewashukuru watendaji na watumishi wa Dawasco
akibainisha kuwa siku hizi simu za malalamiko anazopigiwa na wateja
kuhusu huduma za maji zinazotolewa na Shirika hilo zimepungua sana.
Amesema hali hiyo inatokana na Dawasco kuboresha huduma zake.
Amesema hivi sasa anatumiwa ujumbe mfupi wa kupongezwa kuhusu huduma za
zinatolewa na Dawasco na kulitaka shirika hilo kuendelea kuchapa kazi ya
kutoa ya kuwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
“Hongereni
kwa huduma nzuri mnazitoa kwa wakazi wa mikoa hii. Nyie ndiyo taswira
ya Serikali katika utoaji wa huduma za maji. Bila nyie Ukatibu wa Mkuu
hauna maana kwa mkoa wa Dar es Salaam hata waziri na wizara kwa ujumla,”
amesema Profesa Mkumbo.
Profesa Mkumbo amesema wizara yake haina mipaka katika utendaji kazi na
kwamba ipo wazi kuwasiliana mtendaji yeyote atakayetaka huduma.
SHARE
No comments:
Post a Comment