Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .
SERIKALI
imeongeza masaa ya unyonyeshaji kwa watoto kwa watumishi wa serikali,
mashirika pamoja sekta binafsi ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora
inayotokana na maziwa ya mama.
Hayo
ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu wakati akifungua Wiki ya Unyonyeshaji, amesema kuwa mama
mzazi baada ya kumaliza miezi mitatu ataingia kazini 3:30 na kuondoka
saa 7:30 katika kumuwezesha mama kunyonyesha mtoto bila kuingiliwa na
majukumu ya kikazi.
Ummy
amesema kuwa watendaji wa Umma na mashirika pamoja na taasisi lazima
wafanye hivyo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyonyesha kwa muda
uliowekwa kwa kipindi cha miezi sita.
Amesema
kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo ambao
unatokana moja ni kukosa maziwa ya mama kwa muda mrefu hivyo kuepuka ni
njia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo.
Waziri
Ummy amesema kuwa suala la lishe lazima liangaliwe kwa ukaribu na wadau
wote katika kuweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo ambao unafanya
kudumaa kwa akili.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda
amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika juu ya masuala ya lishe
na wadau kwa mifumo mbalimbali.
Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji wa kina mama ni muhimu katika katika ukuaji wa mtoto wa kumjenga katika afya bora.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini
Mkindo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. Pombe
Magufuli imwemeka kipaumbele katika ubaoreshaji wa lishe nchini.
Amesema
kuwa sera zimeweza kuongezeka katika masuala ya lishe ikiwa eneo la
kipaumbele katika mpango wa taifa wa miaka mitano pamoja mikoa na
halmashauri kuwa na bajeti ya lishe.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akipata maelezo juu masuala ya lishe kutoka kwa mtaalam wa lishe wa
Taasisi ya Chakula lishe nchini (TFNC),Neema Joshua wakati maadhimisho
ya wiki ya unyonyeshaji leo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji na uzinduzi
usambazaji taarifa kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda
akizungumza juu ya mikakati ya lishe na umuhimu wa unonyeshaji leo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo akitoa salamu
za mashirika yasio ya kiserikali yanavyofanya kazi katika sehemu ya
lishe kwa kuwa miradi mbalimbali.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa taarifa kupitia simu za mikoni
katika ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji leo.
Sehemu ya wadau katika ufunguzi wa wiki ya unonyeshaji leo jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment