Naibu Waziri wa
Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi
Kigwangalla (MB),mapema Agosti 17,2017 amefanya ziara ya kutembelea
vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo
Mkoani hapa.
Dk.Kigwangalla ametembelea Kituo cha Afya
Kaloleni, kituo cha Afya Levolosi, kituo cha Afya Ngarenaro, Kituo cha
Afya Daraja Mbili, Kituo cha afya Mkonoo na Kituo cha Afya ambacho
kinajengwa cha Muriet Mpya .
Akizungumza wakati wa kutoa maagizo kwenye
vituo hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V.Timothi
Wonanji na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka
Mundhe na viongozi wengine wa mkoa akiwemo kaimu Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha Rebecca Mongi kuhakikisha wanatatua changamoto za Afya ikiwemo
ukosefu wa vyumba vya upasuaji na ukosefu wa vitendanishi katika mashine
za vipimo vya maabara.
"Mnavyo vituo vya Afya 7. Mnahitaji
kuwekeza zaidi ili mnunue vifaa vya Maabara na kufanyia ukarabati hivyo
vilivyopo. Kuna vifaa vya maabara vya kisasa ambavyo ni ‘portable’ na
havina gharana kubwa. Tunataka mtenge fedha za kutosha ili kuimarisha
sekta ya Afya" aliagiza Dk Kigwangalla.
Aidha akitoa agizo wakati kukagua kituo cha
Afya Daraja Mbili ameagiza mara moja jengo la Chumba cha Upasuaji cha
kituo hicho kianze kazi ndani ya wiki mbili na upasuaji ufanyike ikiwemo
wataalamu kuwapo hapo muda wote.
"Naagiza ndani ya wiki mbili. Huduma za
upasuaji zifanyike hapa kwani mnacho kila kitu , vifaa vingi na vya
kutosha na jengo zuri la kisasa" alisema, Dk Kigwangalla.
Katika hatua nyingine Dk.Kigwangalla
ameagiza kituo cha Afya Kaloleni kuhakikisha wanajenga wodi ya akina
mama na kukamilisha maboresho ya Chumba cha upasuaji.
"Hiki kituo hakina hadhi ya kuwa Kituo cha
Afya. Ni sawa na Zahanati tu maana kama hakuna huduma muhimu za
upasuaji na wodi ya wazazi, nahitaji kuona munakamilisha mara moja"
alieleza Dk. kigwangalla.
Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla
ameweza kukagua sehemu za Maabara, wodi za wazazi na vyumba vya upasuaji
pamoja na maeneo mbalimbali ya hospitali kuona utendaji wa kazi muhimu
na namna ya utoaji wa huduma zinazotolea katika Jiji la Arusha.
Mbali na kukagua vituo hivyo vya Arusha, Dk.
Kigwangalla pia ameweza kutembelea baadhi ya maeneo yanayotarajiwa
kujengwa vituo vya Afya kwenye maeneo hayo ya Wilaya ya Arusha.
Naibu Waziri wa Afya,
Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla
(MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa Kituo cha Afya Kaloleni namna
watakavyojenga wodi ya Wazazi katika moja ya maeneo ndani ya kituo hicho
cha Afya Kaloleni, Wilaya ya Arusha, mapema Agosti 17,2017 wakati
wa ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea
utendaji kazi katika sekta hiyo ya Afya Mkoani hapa.
Naibu Waziri wa Afya,
Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla
(MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa kituo cha Afya Levolosi juu ya
uwekaji wa vifaa vya Maabara hiyo
Dk. Kigwangalla akkagua chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Levolosi
Dk. Kigwangalla
akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati
akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk. Kigwangalla
akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati
akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk.
Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi
wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro. Kulia kwake ni
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V. Timothi Wonanji na kushoto ni Kaimu
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akiwa
katika kituo cha Afya Themi wakati wa ziara yake hiyo. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya kinachojengwa wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya Jiji la Arusha wakati wa ziara yake hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati alipotembelea kituo cha Afya
Kaloleni.
Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dk. Kigwangalla
akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Rebecca Mongi
wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua vituo vya Afya
SHARE
No comments:
Post a Comment