Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa
maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya Hari Singh & Sons, Jaspal
Singh (kushoto), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya
Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 kwa kiwango cha
lami, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Hari Singh & Sons, Jaspal Signh, akitoa ufafanuzi kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani,
kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo
Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 kwa kiwango cha lami, jijini Dar es Salaam.
Muonekano
wa sehemu ya barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu
wa KM 2.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, ambapo ujenzi wake umefika
asilimia 57.
Mhandisi
wa miradi kutoka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Ngusa
Julius, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.
Edwin Ngonyani, ramani ya Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15
kila upande linalojengwa na Kampuni ya Milembe & Kika JV eneo la
Kawe, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Milembe & Kika JV anayejenga
Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15 kila upande, lililoko
barabara ya Mwai Kibaki, wakati akikagua ujenzi wake, jijini Dar es
Salaam.
Muonekano
wa sehemu ya chini ya ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita
15 kila upande, lililoko barabara ya Mwai Kibaki, jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………….
Serikali
imetoa siku 60 kwa mkandarasi wa Kampuni ya Hari Singh & Sons
kumaliza ujenzi wa kipande cha barabara cha kilomita 1.5 kilichobaki kwa
kiwango cha lami katika barabara ya Kimara Baruti-Msewe-Chuo Kikuu
yenye jumla ya urefu wa kilomita 2.6.
Akitoa
agizo hilo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha
kuwa anamaliza mradi huo haraka na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba
ili idumu kwa muda mrefu.
“Ikifika
mwezi Oktoba nataka unikabidhi barabara hii ikiwa imekamilika kwa
kiwango cha lami na vigezo vinavyokubalika, amesisitiza Eng. Ngonyani.
Aidha,
Naibu Waziri Ngonyani amefafanua kuwa mkandarasi huyo hatoruhusiwa
kutekeleza mradi mwingine wa barabara nchini endapo atashindwa
kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati.
Kwa
upande wake Mhandisi Mradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),
Eng. Ngusa Julius, amesema kuwa TANROADS tayari imeshatoa notisi kwa
mkandarasi huyo kuwa kama hatakamilisha kazi ya ujenzi ndani ya muda wa
mkataba hatua za kudai fidia kulingana na mkataba zitafuata na baadae
kukatisha mkataba.
Ameongeza
kuwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unasimamiwa na TANROADS kupitia
kitengo chake cha wahadisi washauri wazalendo (TECU) na unagharimu
shilingi Bilioni 5.7 ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia mia moja.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amekagua daraja la Mlalakuwa
lenye urefu wa mita 15 kila upande, lililopo barabara ya Mwai Kibaki
jijini Dar es salaam na kusisitiza kwa mkandarasi Milembe & Kika JV
kuhakikisha anamaliza ujenzi wa daraja hilo kwa wakati.
Ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa unagharimu shilingi Bilioni 4.8 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwakani.
SHARE
No comments:
Post a Comment