Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea
akizungumza na Wanafunzi wa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi
jijini Dar es Salaam wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa vyumba vya
madarasa ya shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za
Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na
Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa
mbunge huyo
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaaa wa
Mwongozo , James Gointamile(CCM), akimuonyesha Mbunge wa Ubungo, Mhe.
Saed Kubenea (CHADEMA), Baadhi ya Vigae ambavyo vilikuwa vinavuja katika
madarasa matatu ya Shule ya Msingi Makuburi mara baada ya Mbunge Huyo
kutoa Milioni 17 kwa ajili ya kununua bati mpya za kisasa kuezeka shule
hiyo.
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea
akionyesha Sehemu ya Paa ambayo inavuja inatarajiwa kuzibwa hivi
karibuni na Mabati amabyo yametolewa kwenye fedha za mfuko wa Jimbo
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea
akiangalia sehemu ya Shimo la choo cha Matundu 12 knachotaraji kujengwa
na fedha za Halmashauri ya Manispaa ya ubungo mara baada ya Choo cha
shule hiyo kutokuwa katika hali nzuri
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea
akizungumza na Walimu wa shule ya Msingi Makuburi mara baada ya
kutembelea chumba cha Walimu
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea Akiwa katika korido za shule msingi Makuburi
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makuburi
SHARE
No comments:
Post a Comment