
NI wiki
nyingine ninapokukaribisha mpenzi msomaji wangu katika ukurasa huu
mzuri. Leo ningependa tujadiliane kuhusu jambo hili ambalo kwa kiasi
kikubwa linawahusu wanaume ingawa wanawake nao wanapaswa kuelewa hali
halisi. Kama wewe ni mume, mchumba au upo kwenye mapenzi ya kudumu na
mwanamke fulani, unaelewa mwanamke wako anahitaji nini kutoka kwako?
Tukiulizana
swali hili harakaharaka, majibu ambayo wengi watayatoa, huenda kwa
kiasi kikubwa yatakuwa yakifanana. Wengi wanaamini kwamba mahitaji ya
msingi ya mwanamke ambaye yupo kwenye uhusiano, ni huduma za kila siku,
ikiwemo chakula, mavazi, fedha na malazi pamoja na kutimiziwa haja zao
za kimwili.
Wengine
wanaamini kwamba hitaji kubwa la mwanamke, ni pesa, yaani wewe mpe pesa
za kutosha atatulia na wewe. Wengine wanafikiria kwamba labda ukimjengea
mwanamke nyumba, ukamnunulia gari au ukimsomesha, basi hapo unakuwa
umemaliza kazi.
Hata
hivyo, uchunguzi wa muda mrefu wa wataalamu wa masuala ya uhusiano,
unatoa majibu tofauti kabisa na kile watu wengi wanachokielewa au
wanachokiamini. Matokeo yake, wanawake wengi wanakuwa wanakosa kile
ambacho ndicho hasa wanachokihitaji kwa wenzi wao ndiyo maana matukio ya
usaliti yamekuwa yakiongezeka kila kukicha.
Mwanamke anahitaji nini kutoka kwa mwenzi wake?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo wanaume wengi hawayajui:
MPE KIPAUMBELE
Ni ukweli
ulio wazi kwamba wanawake wengi wanapenda kupewa kipaumbele katika
mambo yote yanayowahusu waume zao hata kama hawana uwezo wa kusaidia
chochote. Kwa mfano, mwanaume anataka kununua kiwanja au nyumba kwa
ajili ya kuishi yeye, mkewe na familia (kama anayo). Ni jambo zuri
kabisa analolifanya lakini mwanamke asiposhirikishwa akaja kugundua
mwenyewe, atajisikia vibaya sana na huenda hata mapenzi kwa mumewe
yakaanza kupungua kwa kudhani anadharauliwa.Wanawake wengi wanapenda
kushirikishwa katika kila jambo linalowahusu waume zao. Mshirikishe
katika mambo madogo na makubwa hata kama unajua hawezi kuwa na msaada
wowote. Ukimpa nafasi hiyo, atajiona kuwa na nafasi kubwa kwenye maisha
yako na atazidi kukupenda.
MUUNGE MKONO
Mnapoamua kuishi pamoja, mnakuwa kama timu moja ambayo maisha yenu yanategemeana. Im
ekuwepo
kasumba ya mfumo dume kwa kipindi kirefu, wanaume wengi wakiamini kwamba
wanawake ni watu dhaifu ambao hawawezi kuwa na mchango wowote kwa
familia zaidi ya kutunza nyumba na kulea watoto. Haya ni makosa makubwa
wanayoyafanya wanaume.
Mkeo
anapokuja na wazo kwako, muunge mkono na mtie nguvu ili aone kama
anaweza kufanya mambo makubwa. Pale anapokwama mshike mkono na muonyeshe
njia, iwe ni kwenye biashara, kwenye kazi au kwenye mambo yake binafsi
au ya familia. Muunge mkono, hiyo itasaidia sana kumf a n y a a o n e
umuhimu wako na atazidi kukupenda.
MSIFIE MARA KWA MARA
Ni ukweli
usiopingika kwamba kihaiba, wanawake ni watu wanaopenda sana kusifiwa,
hasa na waume zao au watu Wanaume wengi huwa na tabia ya kuwasifia wenzi
wao katika siku za mwanzo za uhusiano wao lakini wakishazoeana, huacha
kabisa. Usiache mkeo akasifiwe barabarani wakati wewe ndiye mwenye
wajibu wa kumsifia.
MSIKILIZE, MPENDE
Wanawake
wengi wanapenda kusikilizwa hata kama wanachokizungumza hakina maana.
Anaweza kuwa anakusimulia habari za mashoga zake, watoto wa jirani au
kuhusu filamu au tamthiliya anayoipenda. Msikilize na changia mazungumzo
yake kuonesha mpo pamoja, hiyo itamfanya azidi kukupenda zaidi na
kujisikia amani akiwa na wewe
Baadhi ya
wanaume huwa na kawaida ya kuwakatisha mazungumzo wenzi wao kwa kuona
hayana maana au kuwa bize na mambo mengine, kwa mfano kuchezea simu au
kuangalia TV wakati wenzi wao wakiwaongelesha. Mwisho muonyeshe kwamba
unampenda na mara kwa mara mtamkie kwamba unampenda.
Nakupenda
ni neno dogo lakini lenye umuhimu mkubwa katika uhusiano wa watu wawili
walioamua kuishi pamoja. Kubwa na muhimu zaidi, hakikisha unamridhisha
muwapo faragha. Ukifanya hivyo, maumivu ya mapenzi utayasikia kwa
wenzako tu. TUKUTANE WIKI IJAYO.
Na: HASHIM AZIZ| Champion Ijumaa
SHARE
No comments:
Post a Comment