TRA

TRA

Saturday, August 5, 2017

MCHEZAJI WA ARSENAL ANATUA DAR

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Beki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell.
 
BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell anatarajiwa kutua nchini leo Jumamosi mchana kwa mwaliko wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.Campbell ambaye pia amewahi kuichezea Tottenham Hotspur ya England, akiwa nchini kesho atajumuika na baadhi ya wadau wa soka kutazama mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba, akiwa nchini Campbellpia atafanya mafunzo kwa timu ya Magnet kwenye Uwanja wa Gymkhana na kutembelea timu ya Muungano.
“Huyu ni nyota wa pili wa zamani wa soka baada ya Leon Osman wa Everton, tunajua bado watu wanakumbuka ujio wa Everton huu ni muendelezo wa kampuni yetu kuleta hamasa ya soka nchini,” alisema Tarimba.Tarimba alisema SportPesa inaendelea kuwapa hamasa ya soka Watanzania kwa ujio wa nyota huyo ukiachana na udhamini iliyoutoa kwa Simba, Yanga na Singida United.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger