
Mwili wa marehemu ulikutwa nyumbani kwa
mganga wa jadi aitwaye Ashura Mkanga mwenye miaka 33 na mkazi wa
kitongoji cha Chang’ombe.
Inaelezwa kuwa mazingira ya tukio yanaonesha kuwa mganga huyo wa jadi
asiye na kibali kuendesha shughuli za tiba asili analaza wagonjwa
nyumbani kwake, anafanya matambiko, anapiga ramli chonganishi, anafanya
tohara za watoto katika nyumba yake pamoja na matambiko.
“Tukio hili ni baya na halikubaliki hapa Dodoma na mahala popote, ni
fedheha kubwa sana kwa wananchi kuendelea kukumbatia imani za
kishirikina katika karne hii na serikali imesogeza huduma za afya karibu
na jamii lakini bado wapo watu hawataki kwenda hospitali na kukubali
kuuawa kwa fedheha na waganga wachonganishi”, alisema Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa wakati akiongea na waandishi wa habari
SHARE
No comments:
Post a Comment