Vigogo
watano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wamefikishwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
TAKUKURU wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara
ya takriban Milioni 275.
Vigogo
hao wa zamani waliyofikishwa Mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Lusekelo Kasanga, Mkurugenzi wa Fedha,
Robert Shemhilu, Harun Mattambo, Godson Makia, Ofisa Ugavi, msambazaji
kutoka kampuni ya M/S Young Dong Electronic Co. Ltd Martin Simba pamoja
na Mwanasheria wao.
Hata
hivyo, Wakili wa serikali Vitalis Peter amewasomea mashtaka mawili ya
uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambapo amedai
kuwa kati ya Januari na Desemba 2011 katika Ofisi za Tanesco Ubungo,
washtakiwa wakiwa waajiriwa wa Shirika hilo, walitumia madaraka yao
vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin Simba bila ya
kufanya uhakiki na kuisababishia serikali hasara ya takribani Milioni
275.
SHARE
No comments:
Post a Comment