Korea
Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha
Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya
kivita kati yake na Marekani yakiendelea.
Vyombo
vya habari vilisema kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan
na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa
mpango huo utaidhinishwa na Kim Jong-un.
Korea ilipuuzna onyo la Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali.
Marekanai imeionya Korea Kaskazini ikisema kuwa vitendo vyake vinamaanisha kuwa huo utakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo.
Waziri
wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis alisema kuwa Korea Kaskazini
itapigwa vibaya ikiwa itaingia vitani na Marekani na washirika wake.
Korea
Kaskazini ilitangaza siku ya Jumatono kuwa inachora mipango ya kufanya
mashambulizi ya makombora katika kisiwa kilicho bahari ya Pacific cha
Guam kilicho na kambi za jeshi la Marekani na watu 163,000
Taarifa
iliyotolewa baadaye ilisema kuwa jeshi litakamisha mpango huo ifikapo
katikati mwa mwezi Agosti na kupeleka kwa kiongozi wao Kim Jong-un
kuidhinishwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment