Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akizungumza wakati akifungua
mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mjini hapa jana.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo
(OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya
Mtwara, Joseph Tesha, Kaimu Katibu Tawala, Francis Mkuti na Mshauri wa
Kilimo Mkoa wa Mtwara, Ally Linjenje.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara, George Mrisho, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wakijitambulisha kwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mkutano na maofisa ugani ukiendelea.
Mafunzo yakitolewa.
Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney, akitoa mada kuhusu matumizi ya bioteknolojia na sayansi katika kilimo.
Ofisa Kilimo Mohamed Kaid kutoka wilaya hiyo, akichangia jambo.
Ofisa Kilimo kutoka Kata ya Msanga Mkuu, Maonyesho Bakari Said, akichangia katika mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo Hamidu Ndago kutoka wilaya hiyo, akichangia jambo.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Mtwara, Joseph Tesha, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo,
Naliendele Mtwara, Benadetha Kimata, akitoa mada kuhusu kilimo bora cha
mhogo.
Wawezeshaji wa mafunzo ya kutumia teknolojia katika kilimo kutoka
COSTECH wakiwa kikazi zaidi katika mafunzo hayo. Kutoka kulia ni
Mtafiti, Dk.Nicholaus Nyange, Rose Soloka na Bestina Daniel.
****
MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema vipindi vya kilimo katika
vyombo vya habari vitasaidia kuinua sekta ya kilimo nchini.
Mmanda ameyasema hayo mjini hapa jana wakati akifungua mafunzo ya namna
ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa
ugani kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mtwara na Halmashauri ya Manispaa
ya Mtwara ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo
(OFAB).
" Nitoe mwito kwa wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na Costech
kuandaa vipindi kwa njia ya radio na televisheni na machapisho
mbalimbali kama magazeti ili kuhamasisha kilimo bora jambo
litakalosaidia kuinua sekta ya kilimo hapa nchini na vijana wataweza
kujifunza kuhusu kilimo badala ya kuangalia vipindi vya visivyo na tija
hasa katika wakati huu wa nchi yetu kuelekea katika uchumi wa viwanda"
alisema Mmanda.
Katika hatua nyingine Mmanda amewataka maofisa ugani katika wilayani
wajenge mazoea ya kwenda kushinda na wakulima mashambani ili waweze
kutoa utaalamu ambao utawezesha kupatikana kwa mazao mengi na bora.
Alisema haiwezekani mkulima kupata mazao bora bila kupatiwa ushauri na
ofisa ugani na hivyo akasisitiza kuwa watalamu hao waache tabia ya kukaa
maofisini, badala yake wakafanye kazi waliyoajiriwa ambayo ni kutoa
ushauri kwa wakulima.
Mmanda alisema kilimo ni sayansi, hivyo kuna haja ya wagavi kupatiwa
mafuzo ya mara kwa mara kutoka kwa watafiti ambao wamekuwa wanafanya
tafiti mbalimbali za namna ya kuboresha kilimo huku akisisitiza
ushirikiano kati ya mkulima, ofisa ugani na mtafiti kuwa ni muhimu.
Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney aliwaambia maofisa ugani hao
kuwa wameamua kutoa mafuzo hayo kwa kuwa wanaamini kwamba changamoto
zinazokabili kilimo ni nyingi hasa magonjwa ya mazao, wadudu waharibifu
pamoja na kukosekana kwa mvua za kutosha.
Alisisitiza kuwa mkulima ili aweze kuwa na kilimo chenye tija, lazima
uongezee udongo wako lishe, utibie mimea yako kama wewe unavyotibiwa na
dawa ili yapone na yatoe mazao mengi. Alisema sayansi ipo kwa ajili ya
kumfanya mkulima apate mazao mengine na sio kuendelea kuwa maskini kama
ilivyo sasa.
“Tuko hapa kuelezea namna teknolojia hizi ambazo zinasaidia kukabiliana
na changamoto hizo, lengo ni kutaka wakulima wetu wazalishe kwa tija
nchi ijitosheleze kwa chakula lakini pia mkulima auze mazao yake na
kupata faida,” alisema Dk. Mneney.
Na Dotto Mwaibale, Mtwara
SHARE
No comments:
Post a Comment