
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua
Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya
Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar
es salaam.Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati
ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
KaimuJajiMkuuwa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim JumaakifunguaPaziakuashiriauzinduziwa
Mahakamaya Watoto (Juvenile Court) leojijiniMbeya.
KatikatiniMwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie
ShanlernakushotoniJajiKiongoziwaMahakamaKuuya Tanzania Mhe. Ferdinand
Wambali.
……………………………………
Na Lydia Churi-Mahakama
Mahakama
ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa
haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri
Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa
miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto
kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.
UtekelezwajiwahakizaWatoto
zilizoainishwakatika mikatabambalimbali yakikandana Kimataifa na kupewa
nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba
21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za
watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni,
Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court)
katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili
hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es
salaam.
Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto
Kwa
kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote,Mahakama ya
Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa
(UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za
watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya.
Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama
ya watoto pekee kwa Tanzania bara. Akizindua jengo hilo hivi karibuni,
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo
haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapanayakesasa,basi azmayamaendeleo
endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini.
AkinukuuandikolaShirika
la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kuwa“Maendeleo
Endelevu yanaanza na kukamilika kwamisingi ya watoto kuwa salama,wawe ni
wenye afyabora na waliopata elimu bora” (Sustainable Development starts
and ends with safe, healthy and well-educated children- UNICEF, May
2013). Katika nenolakelautangulizikatikaandikohilo,
AnthonyLake,Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF aliandika kuwa:Hakizawatotona
afya yaonjema, lazimaipewe kipaumbele katika maandalizi ya
ajendayamaendeleoendelevuya baadayamwaka2015. Uwekezaji kwa manufaa ya
watoto ni njiaborayakufutaumaskini,kuongezakasiyakuchanua kwa manufaa
kwa wote.” Alisema andiko hilolinatukumbusha kuwa ustawi wa Watanzania
unaanza na Ustawi wawatoto.
Ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto
Kaimu
Jaji Mkuu aliendelea kusema kuwa maana ya ustawi wa watanzania unaanza
na ustawi wa watoto ni kwamba tayari Katiba imetamka kuwa lengo kuu na
jukumu la Serikali ni ustawi wa wananchi na ustawi huo wa wananchini
lazimaujengewe misingi imara ya ustawi wa watoto wa leo.
Alisema
jamii ya watanzania bado inayo mengi ya kufanya ili kuendeleza asilimia
50 ya wananchi wake ambao wana umri wa miaka 18 na chini ya miaka hiyo.
Alisema,kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti
mwaka 2012, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na idadi ya watu
milioni 44,928,923 na kati ya hao, watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0
hadi 17ni asilimia 50.1
Mikataba ya Haki za Watoto iliyoridhiwa na Tanzania
Kutungwa
kwa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 nchini Tanzania kunatokana
na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayotambua na kulinda haki za
Watoto ambayo Tanzania iliridhia. Baadhi ya Mikataba hiyo ni Mkataba wa
KimataifawaHakizaMtoto (UNConvention on the Rights of the Child -UNCRC),
Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (African Charter on the
Rights andWelfareoftheChild-ACRWWC). Mikataba mingine ni ule wa United
Nations Standard Minimum Rules for theAdministration of Juvenile Justice
(Beijing Rules) na United Nations Guidelines for the Prevention of
JuvenileDelinquency (The Riyadh Guidelines).
Matokeo Ya Kutungwa Kwa Sheria Ya Mtoto ya mwaka 2009
Tanzania
ilitunga Sheria ya Mtoto Namba 21 ya 2009 kwa ajiliya haki, ulinzi na
ustawi wa mtoto. Aidha, Sheria hii imekusanya mapendekezo yoteya ndani
yanchi, ya kikanda naya kimataifa kuhusumaboreshoyahaki na maslahi
mapana ya mtoto na kutoa nguvu yakisheria. Baada yakutungwakwaSheria
hii, mihimili yadolaimepewa majukumu ya kutekeleza na kuwajibika. Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania anasema kwa upande wa
mhimiliwaMahakama,inategemewaMahakamayaWatotoisaidiekuwajibikanakutekelezaSheriayaMtoto.
Alisema
kunamaeneokadhaakatikaSheriayaMtotoambayo
yanasimamiwanamamlakanyingine.Pamojana ukweli huo,badoMahakamaya
Watotoinawezakutoa
ushirikianokwamamlakahizoauamrizamahakamazikasaidiautendajiwa mamlaka
hizo, kwa mfano; mazingira mbalimbali ambayo yameainishwa na SheriaNamba
21 ya 2009 kuwa ni hatarishi kwa mtoto kama vile uyatima, kutelekezwa,
kuteswa, kuzurura, kukinzanana sheria ambapo alisema Mahakama ya Watoto
inaweza kutoa tafsiri nakupanua wigo wa “mazingira hatarishi”. Mahakama
ya Watoto inaweza kutoa tafsiri nakupanuawigowaUlinzina
wajibuwawazazikwamatunzo ya mtoto,matibabu na elimu, sifa za mtu kuwa
mlezi na uasili wa mtoto; namna gani Mahakama itawasilisha taarifa mbali
mbali aukutumia rejista ya watoto walioasiliwa kwa Msajili waVizazi na
Vifo pamoja na uzuiaji wa kazi za udhalilishaji kwa watoto wenye umri wa
chini ya miaka18.
rof.
Juma alisemaMahakamaya Watoto inaweza kutakiwa kutoa miongozokuhusu
mafunzo ya kazi (apprenticeship) kwa watoto chiniya miaka 18 na
kuchunguza mikataba ya mafunzo ya kaziambayo ni kandamizi au
yasiyozingatia maslahi ya mtoto. MahakamayaWatoto pia
inawezakutoamaamuziambayo yatazikumbushaSerikali zaMitaa
wajibuwaowakuboresha ustawi wa watotowaliondani ya mamlakazaSerikali ya
Mtaa husika. Mahakama inaweza kuitahadharisha Serikali Kuu naSerikali za
Mitaa na Halmashauri wajenge shule maalumza watoto za kutosha. Hii
itasaidia Mahakama ya Watotokuwa,badala
yaadhabuyavifungogerezani,watotowaliopatikana na hatia watapelekwa.
Kwakuanzisha nakuendesha Shule, Mihimili mingine nayo itakuwa
inaisaidiaMahakama na Magereza kutekeleza wajibu wao kwamujibu wa Sheria
Namba 21 ya 2009.
Aidha
Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zitakapoanzisha vituo vya kutunzia na
kulelea watoto wenye shida ya malezi na Bunge kutoa fedha za kutosha
kuendesha vituo hivyo zitaisadia Mahakama kwa kiasi kikubwa, alisema
Kaimu Jaji Mkuu na kuongeza kuwa MahakamazaWatotopia
zinawezakugunduamapungufukatikaSheriana kupendekezakuwa Waziri
mwenyedhamana ya watoto atunge kanuni stahiki.
Sheria ya Mtoto Shirikishi nainataka Ushirikiano
Akizungumzia
ushiriki na ushirikishwaji wa Sheria ya Mtoto, Kaimu Jaji Mkuu alisema
Sheria kuwa sheria hii imesimamakatika misingi ya ushirikiano baina ya
mihimili yote, ushirikianona wadau mbali mbali kama UNICEF na NGOs,
taasisi ambazo zinashughulika na masuala ya haki za watoto. Alisema,
Sheria hii pia inaitaka Mahakama ichukue uongozi, na kunamasuala ambayo
mihimili mingine imepewa nafasi ya uongozi hivyo Mahakama inayo nafasi
nzuri ya kuipa uhai sheria hii kwa kuwa kwanza, haki zote stahili
zilizoainishwa ndani ya Sheriahii zinamfaidisha mtoto, pili, Sheria hii
inapotafsiriwa,paleambapo wanaona kuna “kutofahamika, “utata” wawena
ujasiri wa kuielekeza sheria kufikia malengo mazuriyaliyowekwa na
Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusuhaki ya watoto.
Mahakama
pia inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai Sheria hii kwa sababu Mahakimu
katika Mahakama ya Watotowatakuwa na nafasi ya karibu kabisa kuona
namnavifungu mbali mbali vya Sheria hii vinavyofanyakazi, hivyo Kaimu
Jaji Mkuu aliwaagiza Mahakama wanaosikiliza kesi za Watoto
kuorodheshamapungufu ya Sheriahiina kuhyawasilisha kwenye kamati ya
Kanuni ya Jaji Mkuu kwa ajili ya kupendekezakwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kuhusu mabadiliko yaSheria.
Akisisitiza
juu ya kulinda haki za Watoto, kaimu Jaji Mkuu aliwataka mahakamu
wanaosikiliza kesi za Watoto wasome taarifa za Utekelezaji
zinazowasilishwa na Tanzania na pia zile zinazowasilishwa na mataifa
mengine kuhusu Tanzania ili waweze kugundua mapungufu yetu ya
kiutekekezaji ili tuweze kupanga namna ya kuboresha utekekezaji.
Mahakimu hao pia wametakiwa kufuatilia haki za Watoto pindi wanapofanya
ukaguzi kwenye Magereza.
Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto Mbeya
Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya
Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania
Milioni
415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF
shilingi milioni 201. Jengo hili lilianza kutumika April 18, 2017 na
linaofisi mbili za Hakimu, Ofisi ya Wakili wa Serikali, ofisi ya Afisa
Ustawi wa Jamii na chumba cha Mawakili wa Kujitegemea.
Sababu za Mahakama kujengwa Mbeya
Jengo
hili ambalo ni la pili la Mahakama ya Watoto nchini limejengwa jijini
Mbeya kwa kuzingatia upatikanaji wa wadau na huduma zote muhimu za haki
kwa mtoto. Huduma hizo ni pamoja na uwepo wa shule ya maadilisho
(approved school) ikiwa ni pekee nchini, kuwepo kwa Mahabusu ya watoto
mkoani humo, na kuwepo kwa dawati la jinsia la watoto lenye viwango
vinavyotambulika lililoanzishwa na Jeshi la polisi. Mahakama hii pia
ilianzishwa kutukana na uwepo wa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto
(child protection team) na kuwepo kwa mfumo wa marekebisho ya tabia kwa
watoto (community rehabilitation programme).
Ushirikiano wa Mahakama na UNICEF katika masuala ya haki ya Mtoto
Katika
kipindi cha takribani miaka mitano yaani tangu mwaka 2012, UNICEF na
Mahakama walishirikiana katika kutengeneza kanuni za Mahakama yaWatoto
ikiwa ni matakwa ya kifungu cha 99(1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009
ambacho kinamtaka Jaji Mkuu kutengeneza kanuni za kutumika katika
uendeshaji wa kesi katika Mahakama za Watoto.
UNICEF
ilitoa msaada wa kitaaluma (technical support) na fedha katika kuandaa
kanuni ambazo zilitangazwa katika Gazeti la Serikali No 182/2016.
Uandaaji wa kanuni hizo ulihusisha wadau mbalimbali wa haki za watoto
kama Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, na
Mashirika yasiyo ya kiserikali vinayotoa msaada wa kisheria na vyombo
vingine vinavyohusika na masuala ya mtoto.
Aidha,
UNICEF imeshirikiana na Mahakama katika kuandaa mafunzo kwa wakufunzi
(TOT) juu ya uendeshaji wa kesi za watoto kwa mujibu wa Sheria na kanuni
za watoto.Wakufunzi walitoka Mahakamani, Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Idara ya Ustawi wa
Jamii.
UNICEF
pia imeshirikiana na Mahakama kutoa mafunzo kwa Mahakimu, Mawakili, wa
Serikali na Waendesha Mashtaka, Maafisa Ustawi wa Jamii, taasisi
zinazotoa msaada wa kisheria na Taasisi zisizo za Kiserikali katika Mkoa
wa Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, na Iringa. Aidha mafunzo kwa wadau wote
yanaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali kwa kutumia wakufunzi
waliopata mafunzo yaliyotolewa na UNICEF na Mahakama.
Kwasasa
Mahakama na UNICEF watashirikana katika kutengeneza rejista za maalum
mashauri ya watoto, kupitia mwongozo wa mafunzo (Training Manual) kwa
kushirikiana na Chuo cha Mahakama Lushoto na Taasisi ya Mafunzo ya
Uanasheria kwa vitendo (Law School of Tanzania).
Sambamba
na hilo kwa mwaka huu wa fedha UNICEF wataendelea kushirkiana na
Mahakama katika mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa wadau wote wa haki
za Watoto. Pia UNICEF imeonyesha nia ya kushirikiana na Mahakama katika
ukarabati mdogo wa Mahakama ili kuziweka katika mazingira rafiki kwa
watoto.
Hata
hivyo, bado iko haja ya kuongeza idadi ya Mahakama za watoto nchini
kutokana na kuwepo kwa kesi za watoto na nyingine ambazo kwa namna moja
au nyingine zinawahusisha watoto katika mikoa mbalimbali nchini ili
kutekeleza azma ya kulinda na kutetea haki za Mtoto.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya watoto jijini Mbeya, Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali aliiomba UNICEF
kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya Mahakama za
watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia
Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto
zinavyofanya kazi.
SHARE
No comments:
Post a Comment