Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani
(Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia Mashine za BVR.Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura alipotembelea
Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati ni
Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA
wa Tume Bi. Mwamvita Solo.
Afisa
TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Julius Kobelsiki akitoa
ufafanuzi kuhusu Mashine ya kuandikisha Wapiga Kura ya BVR kwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji na watumishi wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Ofisi
za Tume jijini Dar es salaam. Kulia kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na Mkurugenzi wa Uchaguzi
Bw. Kailima Ramadhani (kulia).
Na. Aron Msigwa - Dar es slaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye UlemavuMhe.
Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa
kuendelea kusimamia matumizi bora ya rasilimali inazopewa na Serikali na
kuzitaka taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo.
Mhe.
Muhagama ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya
kutembelea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuangalia utekelezaji wa
maagizo ya Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na
Utawala Bora iliyoridhia Bunge lipitishe fedha kiasi cha shilingi
bilioni 10 kuiwezesha Tume kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura nchini .
Akizungumza
na watendaji na baadhi ya watumishi wa Tume amesema kuwa ameridhishwa
na utendaji kazi wao na namna Tume ilivyojipanga kutekeleza jukumu la
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuelekea uchaguzi ujao wa
mwaka 2020 kwa kuwa na mpango Kazi, unaochambua na kubainisha mahitaji
muhimu yanayotakiwa, lini na wapi ili kazi hiyo iweze kufanyika kwa
umakini.
“
Naipongeza sana Tume kwa kuendelea kufanya vizuri , nimegundua kuwa
imejipanga vizuri kutekeleza majukumu yake ambayo yameainishwa Katika
Katiba, kwa niaba ya Waziri Mkuu nimekuja hapa na timu ya watendaji
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati
ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora walioridhia Bunge lipitishe
fedha shilingi Bilioni 10 ili kuiwezesha kufanya maandalizi ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura” Amesema.
SHARE
No comments:
Post a Comment