NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
JUKWAA
la Wahariri Tanzania, (TEF), chini ya uenyekiti wake, Bw.Theophile Makunga,
limetangaza kuondoa adhabu ya kutoandikwa habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mhe. Paul Makonda,(pichani juu), kuanzia leo Agosti 9, 2017.
Akitangaza
uamuzi huo kwenye hoteli ya Holyday Inn katikati ya jiji la Dar es Salaam leo Agosti
9, 2017, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), Bw. Theophil Makunga
aliyefuatana na Makamu wake, Bw. Deodatus Balile, Katibu Mkuu, Bw. Neville
Meena na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TEF, Bw. Bakari Machum, alisema, baada ya
vikao mbalimbali vilivyofanyika baina ya Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam na
TEF, wameona ipo haja ya swala la adhabu aliyowekewa Mkuu wa Mkoa kufikia
kikomo.
TEF
ilivitaka vyombo vya habari vya Radio, Televisheni, Magazeti na Blogs,
kutoandakia habari za Mkuu huyo wa Mkoa, kufuatia kile kilichoelezwa kuwa Mkuu
wa Mkoa Mhe. Paul Makonda, aliingia kwenye studio za Clauds Media Group, (CMG),
usiku wa Machi 18, 2017, akiwa na walinzi wake waliobeba bunduki, kitendo
kilichotafsiriwa na wamiliki wa kampuni hiyo kuwa ni uvamizi.
Hata
hivyo TEF, katika mkutano huo na waandishi wa habari imesema, kumekuwepo na
mazungumzo ya muda kidogo baina ya Jukwaa la Wahariri na Mkuu wa Mkoa Makonda
kutafuta suluhu ya swala hilo, lakini wakati swala hilo linakaribia kutafutiwa
ufumbuzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia
wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi
kutoka Hoima nchini Uganda kuja bandari ya Tanga, alimwita Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, (CMG), Bw. Ruge
Mutahaba na kuwataka washikane mikono kama ishara ya kumaliza tofauti zao.
“Kwa
upande wetu sisi kama TEF tumeona hatuna sababu ya kuendelea kumfungia RC
Makonda, wakati tayari Rais amekwisha wasukuhisha watu hawa hadaharani.”
Alisema Makunga wakati wa mkutano huo na Waandishi wa habari.
Kama
bado kuna tofauti ndogondogo baina yao nadhani wataendelea kujadiliana lakini
kwa upande wetu tunasema adhabu imefikia ukomo leo. Alisisitiza makunga.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema, yeye na Clouds wamekuwa na
mahusiano mazuri kwa muda mrefu na kwamba mazingira ya wakati ule alipoingia
kwenye studio za Clouds na walinzi yalikuwa hayaepukiki, kwani walinzi aliopewa
wapo kuhakikisha usalama wake, lakini pia kufuatilia nini anachofanya katika katika
shughuli zake mbalimbali kama Mkuu wa Mkoa. “ Mimi niseme tu kwamba yaliyopita
sindwele tugange yajayo na ninawaomba Waandishi wa habari tuendelee kuwatumikia
wananchi wa Moa wa Dar es Salaam kwa kujenga ushirikiano.” Alisema Mhe.
Makonda.
Katika
mkutano huo pia alikuwepo Bw. Ruge ambaye yeye alisema, haoni sababu ya
kuendelea kwa mgogoro huo kwa vile kama ambavyo kauli ya Rais wa Nchi aliyosema
kwenye mikutano yake kuwa yeye ni dereva na dereva pengine wakati akiendesha
gari amesikia abiria wake wanapiga kelele na ndiyo maana ameamua kuingilia kati
na kwa hali hiyo kwa upande wake anaona ni hatua nzuri ambayo sasa hakuna
sababu tena ya kuendelea kujadiliana na wala hakuna haja ya kuanza kuuliza nani
alikosa na nani yuko sahihi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.
Paul Makonda, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa
habari ulioitishwa na TEF kwenye Hoteli ya Holyday Inn jijini Dar es
Salaam, leo Agosti 9, 2017. Wengine kutoka kushoto ni Bw. Bakari Machum,
Mjumbe wa TEF, Bw. Theophil Mkunga, Mwenyekiti wa TEF, Bw. Deodatus
Balile, Makamu Mwenyekiti wa TEF, na Bw. Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa
Vipindi wa Clouds Media Group, (CMG).
Bw. Theophil Makunga, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), akizungumza leo Agosti 9, 2017.
Bw. Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, (CMG), akizungumza leo Agosti 9, 2017.
Waandish wa Habari wakiwa na "zana" zao.
Waandishi wa Habari
Waandishi wa Habari
Waandishi wa Habari
Katibu Mkuu wa TEF, Bw. Nivelle Meena, akizungumza leo Agosti 9, 2017
Bw. Hamisi Mzee kutoka Baraza la Habari Tanzania pia alikuwepo.
Bw. Balile, (katikati), akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda, (kushoto), na Bw. Ruge Mutahaba
Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda,
(kulia), akipeana mikono na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bw. Ruge
Mutahaba, huku Mwnyekiti wa TEF, Bw. Theophile Mkunga, akionyesha furaha
yake baada ya kumalizika kwa mgogoro huo.
Mhe. Makonda na Bw. Mutahaba, wakiondoka kwenye chumba cha mkutano
Mkuu wa Mkoa Makonda (katikati),
akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa TEF, Bw. Makunga (kushoto) na Makamu
Mwenyekti wa TEF, Bw. Balile.

SHARE
No comments:
Post a Comment