Msanii
wa muziki kutoka mkoani Mwanza, Mo Music amesema msanii mwenzake
Timbulo kusema amemsaidia lakini hakutaka kutangaza hakuwa sahihi, kwani
kusaidiana ni kitu cha kawaida.
Mo
Music amesema anamuheshimu Timbulo kama msanii mwenzake na amemkuta
kwenye game, lakini kitendo cha kusema amemsaidia sana ni uongo na hata
suala la kutangaza anambania, halina ukweli wowote na hajapendezwa
nacho.
“Timbulo
ni kaka kwangu lakini anakuwa anakosea anapozungumza hivyo, kiukweli
amenikwaza, Timbulo ni kaka ambaye nimemkuta kwenye muziki, anavyosema
mimi natangaza ananibania ananibania nini, kwa sababu yeye ana mashabiki
wake na mimi nina mashabiki wangu, hakuna faida yoyote”, alisema Mo
Music.
SHARE
No comments:
Post a Comment