Msanii wa
hip hip Bongo, AY amempongeza msanii mwenzie kutoka nchini Kenya,
Jaguar kwa kuchaguliwa kuwa mbunge katika jimbo la Starehe.
Rapper
huyo amesema ushindi wa Jaguar ameupokea kwa furaha kubwa kwa sababu
anamfahamu zaidi na isitoshe alimtambulisha katika game ya muziki rasmi
pale walipotoa ngoma ya Nimetoka Mbali.Siku ambayo alisema anataka
kuingia kwenye siasa nilishtuka kidogo lakini vitu ambavyo alikuwa
anavifanya ni kama wanasiasa kabisa na pengine hata zaidi, so naamini
jimbo la Starehe wamepata mtu sahihi na nina uhakika atawafanyia mambo
makubwa,” AY amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times Fm na
kuongeza.
“Kwa
upande mwingine inaonyesha ukiwa na nia na kitu na ukakifanyia kazi
utatimiza ndoto zako na utafanikiwa ndio kitu nimejifunza, pia
inaonyesha mtu unaweza ukafanya muziki na jamii ikakukubali kwa upande
mwingine, ukiona mifano kama wakina Mr Two, Professor Jay, Bobi Wine,”
amesema.
AY
ameendelea kusema ameongea na Jaguar na kumtakia kila la kheri na
kumueleza amtangulize Mungu mbele katika kazi yake na vitu alivyoaidi
azidi kutekeleza katika jamii.
SHARE
No comments:
Post a Comment