Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, UVCCM Mkoa wa
Arusha, Lengai Sabaya ambaye ni Diwani wa Sambasha anashikiliwa na Jeshi
la Polisi kwa tuhuma za kughushi na kutumia kitambulisho cha Usalama wa Taifa.
Kamanda
wa Polisi Arusha Charles Mkumbo amesema Sabaya anashikiliwa kwa kosa
alilolitenda awali ambapo Polisi waliliondosha shauri hilo Mahakani kwa
kuwa upelelezi ulikuwa haujakamilika na sasa umeshakamilika.
"Anatarajia
kufikishwa Mahakamani wakati wowote. Ni kosa ambalo alilitenda huko
nyuma na tuliliondosha Mahakamani kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.
Sasa uchunguzi umekamilika na hati iko timamu na atafikishwa Mahakamani.
“Kosa alilokamatwa nalo ni alijifanya Afisa wa Usalama wa Taifa kitendo ambacho si cha kweli, yeye sio Afisa wa Idara hiyo.
“Hatuwezi
kumzuwia mtu kusema chochote lakini ukweli ndio huo na hili shauri
halijatokea leo, lilishatokea kitambo. Ni suala tu la kitaalamu kama
Wapelelezi. Kupeleleza kesi ni ili iwe na mafanikio. Kwa hiyo hilo suala
la watu kusema masuala ya kisiasa sisi sio wanasiasa. Sisi ni watendaji
tunaofanyakazi kwa mujibu wa sheria.” Amesema Kamanda Charles Mkumbo.
SHARE
No comments:
Post a Comment