Rubani wa
Ndege ya Kampuni ya Safari Air Link DH-SAL aina ya Cessna 206 ambayo
ina uwezo wa kubeba abiria watano amefariki baada ya ndege aliyokua
anairusha kuanguka katika maeneo ya Monduli, Arusha.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema jana kuwa rubani huyo aliyetambulika kwa
jina la David Mbale alikuwa akiruka kuelekea Serengeti kwa ajili
kuchukua wageni. Jeshi la Polisi bado linaendelea kuchunguza chanzo cha
ajali hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment