Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amekana vikali madai ya ripoti kuwa anajianda kuwania urais mwaka 2020.
Likinukuu vyanzo tofuati ripoti ya gazeti hilo ilisema kuwa bwana Pence anaweza kuwania Urais ikiwa Trump hatawania tena
Bwana Pence amesema ripoti hiyo ni jaribio la kuvuruga uongozi.
- Marekani yaionya vikali Korea Kaskazini
- Mike Pence na Taro Aso wateta kuhusu Korea Kaskazini
- Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa
"Ni ukweli kuwa makamu wa rais anajiandaa kwa mwaka wa 2020, kuchaguliwa tena kama makamu wa rais," aliliambia Shirika la ABC.
Msemaji wa Gazeti la New York Times alitetea ripoti hiyo akisema wana imani na taarifa zao na wataiacha ripoti hiyo kuijieleza yenyewe.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment