Maafisa wa polisi
wa Uhispania wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils
ili kuzuia jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la hapo awali
kufanyika mjini Barcelona.
Watu 13 walifariki huku makumi wakijeruhiwa baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini Barcelona eneo la Las Ramblas siku ya alhamisi mchana
- Dereva wa gari hilo alitoroka na bado anaswaka.waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy alisema kuwa lilikuwa shambulio la kijihadi.
- Watu 13 wauawa na mamia kujeruhiwa, Barcelona
- Watu 13 wafariki katika baa Ufaransa
- Watu 13 wauawa kwa kupigwa risasi India
- Moto waua watu 13 nchini Ufaransa
Awali afisa mkuu wa polisi Josep Lluis Trapero alisema kuwa inaonekana wakaazi wa eneo la nyumba ya Alcanar walikuwa wakiandaa kuntengeza kilipuzi .
Mjini Cambrils watu saba akiwemo afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa wakati gari lilipovurumishwa katika umati wa watu mapema siku ya Ijumaa kulingana na huduma za dharura huko Catalan.
Mtu mmoja yuko katika hali mahututi.
Vyombo vya habari vya Uhispania viliripoti kwamba washambuliaji waliuawa wakati walipojaribuo kutoroka baada ya gari lao kupinduka.Baadaye misururu ya milipuko ilifuatia.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment