Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati),
akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakati alipofanya kikao cha
pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (Kulia), wakati alipokagua sehemu ya
kuingilia abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNIA), leo jijini Dar es
Baadhi
ya Wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati
alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja,
leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.(PICHA NA WUUM)
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi
mmoja kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kulipa kodi ya Majengo kama
mikataba yao inavyolekeza.
Waziri
Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao
ili kujadili changamoto mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili
kuendelea kutoa huduma bora katika uwanja huo.
“Kulipa
kodi za majengo hapa ni suala la lazima, hivyo ifikapo Septemba
mwishoni nataka kuona wafanyabiaashara wote mmeshalipa kodi ya pango,
makusanyo haya ni muhimu kwetu ili tuendelee na hatua nyingine za
uboreshaji wa viwanja vya ndege na huduma nyinginezo.” Amesisitiza
Profesa Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa ameutaka uongozi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege
Tanzania (TAA), Kuhakikisha mikataba yote ya upangishaji wa majengo
inapitiwa upya na kufanyiwa marekebisho ili thamani ya fedha iendane na
wakati huu.
Profesa
Mbarawa amewahimiza wafanyabiashara hao kubadilika na kuendana na
mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ili kuweza akuendana na ushindani wa
kibiashara uliopo ndani na nje ya nchi.
Ameongeza
kuwa Serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri kwa wafanyabiashara
nchini ili waweze kufanya biashara zao ili kujiingizia kipato binafsi
na kukuza pato la Taifa.
Katika
hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua sehemu ya kuingilia abiria
katika uwanja huo ambapo amesema Serikali itaweka mpango maalum wa muda
mfupi kwa wasafiri wanaoenda nje kutotumia muda mrefu katika ujazaji wa
fomu wakiwa uwanjani hapo.
“Kwa
kushirikiana na taasisi zote zinazotoa huduma katika uwanja huu
tutaweka mpango maalum utakaowezesha wasafiri kuhudumiwa kwa haraka na
kwa muda mfupi, Msafiri yoyote anataka huduma za haraka ili waweze
kuwahi na sisi tutahakikisho tunakidhi mahitaji ya wateja,” amesisitiza
Profesa Mbarawa.
Kwa
upande Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Salim Msangi amesema Mamlaka imeshapitia mikataba yote ya
wafanyabiashara kiwanjani hapo na hatua inayofata ni kufatilia madeni
yote ili kuboresha huduma katika kiwanja hicho.
Bw. Msangi ameongeza kuwa kwa yale madeni ambayo hayataweza kulipwa kwa wakati taratibu za kisheria zitafuatwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment