Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Agosti 7, 2017 imeahirisha kwa mara
nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi nyaraka inayowakabili
Rais wa Simba SC, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange maarufu
Kaburu hadi Agosti 22, 2017 baada ya upelelezi kutokamilika.
Kesi
hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mwambapa baada ya Wakili
wa TAKUKURU, Kishenyi Mutalemwa kueleza kuwa upelelezi haujakamilika na
kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine, ambapo watuhumiwa wamerudishwa
gerezani.
Aveva
na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba
na kutakatisha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na
wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
SHARE
No comments:
Post a Comment