
Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya
Singida United Festo Sanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya
YARA Alexander Macedo wakibadilishana nyaraka za mkataba wa udhamini wa
mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
Matajiri kutoka mkoani Singida
klabu ya Singida United wamefanya mabadiliko kidogo katika safu ya
ushambuliaji katika usajili baada ya kufungwa na Mabingwa wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara Yanga cha magoli 3-2 kwenye Mchezo wa Kirafiki
uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu
huu, imemchukua mshambuliaji Michelle Katsavairo kutoka klabu ya Keizer
Chiefs ya Afrika Kusini kwa mkopo na kumuacha Mzimbabwe mwenzake, Wisdom
Mtasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya
Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya
Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
Hayo yamethibitishwa na
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba baada ya
kusajiliwa kwa Katsavairo kutoka Kaizer, Mtasa anapalekwa kwa mkopo wa
Stand United ya Shinyanga.
Aidha Mkurugenzi huyu amesema kuwa
wamefanya hivyo ili kuweza kusajili mchezaji mwingine wa kigeni japo
kuwa walikuwa wamefikia idada ya wachezaji saba wa kigeni hivyo
imewapelekea kumtoa mchezaji m0ja kwa mkopo.
Singida United mpaka sasa
wameshacheza michezo mitano ya kirafiki wakishinda mechi mbili dhidi ya
Pamba 5-0 na Alliance 2-0 huku wakitoka sare na wanajeshi wa Pwani Ruvu
Shooting ya kufungana goli 1-1 na kupoteza michezo miwili dhidi ya
Lipuli FC kwa kufungwa 1-0 na kufungwa 3-2 na Yanga.

Kocha Mkuu wa klabu ya Singida
Hans Van Der Pluijm akiongea na waandishi wa habari baada ya Kampuni ya
YARA kuingia mkataba na klabu hiyo wenye thamani ya shilingi milioni
250.
Licha ya kufungwa na Yanga ,vijana
wa Hans Van Der Pluijm walicheza kandanda safi na la kuvutia na
kutawala kwa kila kitu na kuwapoteza kabisa viungo wa Yanga tatizo
ambalo lilitakiwa kufanyiwa marekebisho ni la golikipa na tayari timu
hiyo imemsajili mlinda mlango kinda toka kwa Wekundu wa Msimbazi Simba
Manyika Peter ambaye amesaini miaka miwili.
Mkurugenzi
Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga (kushoto) na Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakitia saini karatasi ya
makubaliano ya udhamini wa timu ya Singida wenye thamani ya Milioni 250.
Singida United itatumia uwanja
wake wa nyumbani wa Jamhuri Dodoma kutokana na uwanja wa Namfua bado upo
katika matengenezo makubwa na utakapokamilika timu hiyo itaweza kurejea
katika makazi yake na inatazamiwa kuleta changamoto kubwa kwa timu
kubwa kutokana na kufanya usajili mkubwa huku ikiwa ndio kinara kwa kuwa
na wadhamini wengi kuliko timu yoyote ile Tanzania tangu lingi
ianzishwe.
SHARE








No comments:
Post a Comment