Mwenyekiti
wa Mpira wa kikapu mkoa wa dare s Salaam, Okare Emesi (kulia) akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka
kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni
Mkurugenzi wa Masoko wa chama , Peter Mpangala na kushoto ni Ofisa
Uhusiano wa Startimes, Samwel Gisayi.
Mkurugenzi
wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala (katikati) akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya
Startimes na Sibuka mapema jana jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dare s Salaam Bw. Okare Emesi na kushoto ni
Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi. (Picha Eliphace Marwa –
Maelezo)
NA
AGNESS MOSHI – MAELEZO.
KAMPUNI ya kurusha matangazo kwa njia ya digitali na
waauzaji wa ving’amuzi Startimes na Shirika la utangazaji la Sibuka waidhamini
ligi ya mpira wa kikapu Dar es Salaam (RBA).
Hayo
yamesemwa na Afisa Mahusiano wa Startimes, Samuel Gisayi wakati
akitambulishwa na Chama Cha Mpira wa Kikapu (BD) kwa waandishi wa habari kuwa mdhamini mpya
wa RBA, Jijini Dar es Salaam.
Bw.
Gisayi amesema kuwa udhamini kwa ligi hiyo kwa sasa ni wa muda mfupi, na baada ya kumalizika kwa ligi
ya RBA wako kwenye mazungumzo ya kuwa wadhamini wa mojakwa moja wa mchezo huo
kwa kipindi cha miaka mitano.
“Tumeamua
kudhamini RBA ili kukuza vipaji vya wacheza mpira wa kikapu kwa sababu
Makampuni mengi yamekua yakiwekeza kwenye mpira wa miguu na kusahau mchezo huu
kusaidia wachezaji waweze kuonekana na kusajiliwa kwenye timu kubwa” , alisema
Bw.Gisayi.
Bw.Gisayi
ameongeza kuwa tayari wamefanya mambo mbalimbali ili kuweza kufanikisha
mashindano hayo ikiwemo kuboresha viwanja ambavyo mchezo huo utafanyika na
kudhamini gharama zote za uendeshaji wa ligi hiyo kuanzia mzunguko wapili mpaka
fainali.
“Ukiachana
na uuzaji wa ving’amuzi Startimes inashirikiana na Jamii katika kuleta
maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo michezo ili kuinua vipaji vya
Watanzania” ,alisititiza Bw.Gisayi.
Bw.Gisayi
ametoa wito kwa wafanyabiashara kupeleka matangazo yao kwenye vituo vyao ili
waweze kutangaziwa kwa bei rahisi wakati wa ligi hiyo , pia ametaka wadau
mbalimbali kutoa ushirikiano kwa mchezo
wa mpira wa kikapu kama michezo mingine .
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa habari na Mawasiliano Bw.Peter Mpangala amesema kuwa
wanaimani mchezo huo utafika mbali na
utakua wa kibiashara kupitia udhamini wa startimes na sibuka kwasababu wamepata
kupata fursa ya kuwa na kurusha michezo yao mubashara kwenye televisheni.
“Ukiwa
na kipindi kwenye televisheni unakaribisha wadau wengi zaidi kuudhamini mchezo
na tunategemea biashara kubwa kwa wachezaji”, alisema Bw.Mpangala.
Bw.Mpangala
ameongeza kuwa amefurahishwa na kitendo cha startimes kuwadhamini kwa sababu
kupitia kampuni hiyo ambayo inashirikiana na taasisi ya kubwa inayosimamia
mchezo huo Duniani (FIBA) wataweza
kufikia malengo ya kuufikisha mchezo huo mbali.
Naye
,Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu
Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Okare Emesu amesema kuwa, wana mikakati ya pamoja na
wadhamini hao ili kuufanya mchezo huo uwe wa kibiashara na uweze kufika mbele
zaidi, vilevile ametoa wito kwa wananchi kufuatilia vipindi vya mchezo huo
vitavyoonyeshwa kwenye king’amuzi cha startimes kupitia Tv Sibuka kila siku ya
Ijumaa, Jumamosi na Jumapili saa kumi na mbili jioni.
Ligi
ya RBA kwa sasa ipo kwenye mzunguko wa
pili na baada ya wiki 3 hatua ya mtoano (playoff) itaanza rasmi kuelekea
fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu Uwanja wa Taifa .
SHARE
No comments:
Post a Comment