TRA

TRA

Tuesday, August 15, 2017

TAWI LA EXIM BANK ZANZIBAR LAADHIMISHA MIAKA 20 TOKEA KUANZISHWA KWAKE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

01
Msaidizi Meneja Uhusiano wa Benki ya Exim Ernest Typa akiwakaribisha wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 20 ya Benki hiyo yaliyofanyika katika Tawi lake liliopo mtaa wa Mlandege Mjini Zanzibar. (kulia) Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Fedha Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar Ismail Omar Bai.
02
Baadhi ya wateja wa Exim Bank walioshiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Benki hiyo wakifuatilia sherehe hizo zilizofanyika katika Tawi lao mtaa wa Mlandege Mjini Zanzibar.
03

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya Exim Bank Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar Ismail Omar Bai akikata keki ya miaka 20 ya benki hiyo katika sherehe zilizofanyika Tawini kwao Mlandege Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga Znz.
……………………….
Na Khadija Khamis – Maelezo 15/08/2017.
Mkurugenzi  wa  Fedha  Shirika la Biashara la Taifa  Zanzibar (ZSTC) Ismail Omar  Bai amewataka wafanyabiashara na wateja wa Exim Bank  kuekeza amana zao katika benki hiyo.
Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 20 ya Exim Bank yaliyofanyika katika Tawi  lao lililopo  Mlandege Zanzibar, alisema iwapo  wafanyabiashara na wateja wataendelea kuwekeza  maendeleo ya Exim Bank yatafikiwa kwa haraka .
Alisema katika kipindi cha miaka 20  tokea kuanzishwa   Exim Benk imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilling za kitanzania TirionI 1.5 ikiwa  ni makusanyo ya  amana za  wateja  .
Aidha aliishauri Exim Bank kuimarisha huduma kwa wateja wao ili kuwavutia wananchi wengi zaidi kuweka amana zao na kuwa moja ya benki zenye kuleta ushindani wa kibiashara Tanzania .
Nae Meneja Mkuu wa Tawi la hilo  Frederick Robert Umiro ametoa shukrani kwa wafanya biashara pamoja na wateja kwa kuwaunga mkono na kupata mafanikio makubwa  ya kibiashara .  
Alisema Exim Bank inatowa mikopo kwa wanachama wake ikiwemo mikopo ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wakubwa ambao huweza kukopeshwa kwa riba ya asilimia 18.
 Akizungumzia mikopo ambayo huwapa wateja wao ni yamikopo mikubwa ya  ujenzi wa nyumba usafirishaji bidhaa kilimo utalii na mengineo kwa lengo la kuweza kujikwamua na umasikini
Alisema Exim Bank ilianza  mwaka 1997  ikiwa na tawi moja  la Samora mjini Dar es salaam  na hivi  sasa imeweza  kuengeza  matawi yake kufikia 33 kwa Tanzania jambo ambalo ni maendeleo makubwa kwa Benki hiyo.
Alifahamisha kuwa katika kutanua huduma zake wamefanikiwa  kufungua  matawi matano  Uganda, matano Visiwa  vya Comorro  na matawi  matatu nchini Djibout.
Naye  mmoja wa wateja wa Exim  Bank Bi Asma  Makame ameipongeza Benki hiyo  kwa kuwajali wateja wao na kuwataka kuiengeza huduma ili iwe kivutio kwa wananchi wengi kujiunga .
Akieleza changamoto  wanazokabiiliana nazo ni ushindani wa kibiashara na mabenki mengine ambayo kila moja  hutumia mbinu za kuvuvutia wateja  kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa unafuu katika baadhi ya huduma zao .

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger