Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba
Mashingi akizungumza katika Kongamano la Biashara la Jijini Tanga leo
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba Mashingi wa pili kutoka kushoto akifurahia jambo na mmoja wa washiriki wa Kongamo hilo la Biashara. |
AFISA
Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba
Mashingi amewahimiza wafanyabiashara mkoani Tanga kutumia huduma wanazozitoa
hususani za mikopo ili waweze kukuza mitaji yao na kutanua wigo wa biashara
zao.
Moshingi
aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada katika kongamano la
biashara lililofanyika
katika Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga na kufunguliwa na Waziri wa
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison
Mwakyembe.
Kongamano
hilo la biashara ambalo limeandaliwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN)
katika mkoa wa Tanga lilijumuisha wadau kutoka kwenye taasisi binafsi na za
serikali,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,vijana na
wasomi.
“Niwaambie
tu huduma hizo zinatolewa na benki yetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina
mbalimbali lakini pia niwapongeze uongozi wa TSN kwa kuandaa kongamano hilo kwa
mara nyengine tena katika mkoa wa Tanga”Alisema.
“Lakini
pia nawakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea tawi letu la hapa mkoani
Tanga lililopo mtaa wa Taifa ili muweze kufaidika na huduma mbalimbali
tunazozitoa.
“Kwani
Benki yetu ya TPB imejikita kumsaidia mtanzania wa kawaida kuweza kuinua
shughuli zake za kiuchumi na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu kwa
ujumla “Alisema
Moshingi.
Aidha
pia alisema wanaunga mkono juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali ya awamu ta
tano kuipeleka nchi kwenye uchumi wa
viwanda ikiwemo jitihada za kufufua viwanda vilivyokufa vikiwemo vya mkoani
Tanga.
Hata
hivyo alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutumia fursa za mradi wa bomba la
mafuta uliozinduliwa na Rais John
Magufuli hivi karibuni kuinua biashara zao kwani wao kama benki wapo
tayari kuwasaidia kufikia mafanikio hayo.
Habari kwa Hisani ya
Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
SHARE
No comments:
Post a Comment