
Kamishna wa Uhamiaji- Pasi na Uraia, Gerald Kihinga
*****
DARA ya Uhamiaji nchini imewataka
wananchi kutambua kuwa paspoti siyo kitambulisho ndani ya nchi na kwamba
kisitumike kwa matumizi hayo kwa sababu siyo utaratibu uliopangwa
kisheria ndani ya mipaka ya nchi.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam
na Kamishna wa Uhamiaji- Pasi na Uraia, Gerald Kihinga wakati
alipofanya mahojiano maalumu na gazeti la Habarileo na kuwaomba wananchi
kutambua kuwa paspoti zinazotolewa zinapaswa kutunzwa na kutumika kwa
lengo lililokusudiwa la kusafiria nje ya nchi.
Pia alisema kuwa ikibainika kuwa mtu amepoteza paspoti hiyo kizembe hatopewa nyingine.
Kihinga alisema kumekuwa na maombi ya
kutengenezewa paspoti baada ya kupotezwa, lakini wengi wamekuwa wakitoa
sababu ambazo zinatilia shaka umakini wa mtu kwenye utunzaji wake.
“Naomba mfahamu kuwa paspoti pia
zinazotolewa siyo vitambulisho ndani ya nchi hivyo visitumike kama
vitambulisho na tena si vizuri kutembea nayo kila mahali kama huna
safari ya nje ya nchi.
Paspoti au hati ya kusafiria zinatumika
kama kitambulisho pale unapokuwa nje ya nchi, lakini matumizi yake rasmi
ni ya kukusaidia kuingia na kutoka nchini,” alisema.
Alisisitiza kuwa kitambulisho rasmi cha
Mtanzania anachotakiwa kutembea nacho ni kile kinachotolewa na Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Aidha, kamishna huyo pia ametaka
wananchi raia wa Tanzania kutambua kuwa wanaweza kupata paspoti wakiwa
popote Tanzania na kwa muda mfupi.
Chanzo-Habarileo
SHARE
No comments:
Post a Comment