![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (aliyesimama) akihimiza jambo wakati akizungumzia kukamatwa kwa wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea kusimamia mkopo wa TADB. |

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James
Ihunyo (aliyesimama) akizungumza katika mkutano wa pamoja na wanachama
wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula,iliyopo katika kijiji cha Mkula wilaya
ya Kilombero.

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,
Bw. Adam Kamanda (kushoto) akiongea kwa uchungu kitendo cha wajumbe wa
Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea kusimamia mkopo
wa zaidi ya shilingi milioni 790 zilizotolewa TADB.

Baadhi ya wanachama na wanakijiji wa
kijiji cha Mkula wakifuatilia mazungumzo wakati wa kikao cha pamoja kati
ya Mkuu wa Wilaya hiyo, wawakilishi wa Benki ya Kilimo na wanachama wa
Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula.

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Mkula
wakitoa maoni yao kuhusu kutoridhishwa na kitendo cha kucheleweshwa
marejesho ya mkopo wa TADB.


Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.


Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.
...................................................................................................
Na Mwandishi wetu
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo ameagiza kukamatwa kwa wajumbe
wa bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula kufuatia kuchelewesha kwa
makusudi malipo ya mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB).
Akizungumza
wakati wa mkutano wa pamoja na wanachama wa Skimu hiyo, Bw. Ihunyo
alisema kuwa uzembe wa Bodi hiyo umepelekea kuchelewesha marejesho ya
mkopo wa takribani shilingi milioni 790.
Mkuu huyo wa wilaya aliongeza pia kitendo cha Bodi hiyo inarudisha nyuma juhudi za serikali katika kupambana na umaskini nchini.
“Lengo
la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini
Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma
juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.
Bw.
Ihunyo aliongeza kuwa kuchelewesha kurudisha mikopo hiyo kunakosesha
wakulima wengine kuchelewa kupata fursa hizo za mikopo hiyo nafuu
inayotolewa na TADB ambayo imelenga kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya
Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia
kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam
Kamanda alisema kuwa tangu wapatiwe mkopo huo, baadhi ya wakulima wa
skimu hiyo wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kurejesha mkopo huo
licha ya jitahada za kuwahimiza kurejesha mkopo huo.
Bw. Kamanda alisema kuwa vitendo hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya
“Mheshimiwa
Rais anahimiza watu kufanya kazi kwa bidii sasa vitendo hivi ni kukaidi
maagizo hayo hivyo kupingana na dhana ya hapa kazi tu inayochagiza
kufanya kazi kwa bidii,” alisema.
Bw.
Kamanda aliongeza kuwa Benki ya kilimo imejipanga kuhakikisha
inatekeleza maelekezo ya serikali ya kuwawezesha wakulima nchini kwa
kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye
tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa
fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo
nchini.
Mwakilishi
huyo wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa TADB imedhamiria na
kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta
Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia
upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia
maendeleo ya kilimo nchini.
“Tuna dira ya Kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi
ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha
kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza
umaskini,” alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment