Wanafunzi
wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya Tunduru
Mkoa wa Ruvuma wamefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati
wakichimba mchanga wa kujengea darasa walipokuwa kwenye mafunzo ya
vitendo.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa mkoani Rukwa SACP Gemini Mushi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba wanafunzi waliofariki ni Selina
Selemani Kazembe (12) wa darasa la tatu pamoja na Sofia Sillo (9)
darasa la tatu kwa kusema kuwa watoto hao waliangukiwa kwa kufunikwa na
ukuta wa shimo la mchanga ambao ulikuwa ukitumika kujengea darasa.
Kamanda
Mushi amefafanua kwamba "Kwa mujibu wa taarifa tulizopewa na uongozi wa
shule hiyo wanafunzi hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo
yajulikanayo kama elimu ya Kujitegemea (EK).
Pamoja
na hayo Kamanda huyo amesema jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza
watoto hao katika hospitali ya Mbesa lakini kwa bahatI mbaya wakati
watoto hao wanafikishwa hospitali walikuwa wameshakata roho.
Kwa mujibu wa Kamanda Mushi amesema jukumu la mazishi familia hizo zimeachiwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment