Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyekaa), akimsikiliza rubani Edger Mcha (kulia) wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipokua anamuonyesha jinsi ya kuongoza ndege inapotaka kuruka na kutua kutoka katika kiwanja cha ndege. Mwenyekiti huyo alipata maelezo hayo wakati alipokua katika darasa la kufundishia marubani chuoni hapo. Masauni alifanya ziara katika chuo hicho na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Akiwa chuoni hapo aliangalia ukaguzi wa magari na pia kupata mipango mbalimbali waliyonayo kuhusiana na elimu wanayoitoa ya kuhusiana na usalama barabarani. Aliyevaa koti ni Mkuu wa Chuo hicho, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Profesa Zakaria Mganilwa |
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Matengenezo Temesa, Mhandisi Sylvester Simfukwe (kulia), wakati Mwenyekiti huyo
alipokuwa anatoka kuiangalia Karakana ya Utengenezaji wa Magari iliyopo katika
ofisi za Temesa, Keko, jijini Dar es Salaam. Masauni alisema lengo kubwa la
ziara yake, kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji
wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za
barabarani nchini
Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiangalia mashine ya kukagua magari kwa
njia ya umeme iliyokua inaonyeshwa na Mhandisi Yakubu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA. Katikati ni Meneja wa Karakana ya kutengeneza magari na mitambo
mbalimbali ya Serikali, Julius Humbe. Masauni alifanya ziara katika ofisi hiyo
iliyopo Keko, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza
lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na
Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiiongoza ndege
katika darasa la kufundishia marubani katika Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT)
kilichopo jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la
kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo
ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini.
Akiwa chuoni hapo aliangalia ukaguzi wa magari na pia kupata mipango mbalimbali
waliyonayo kuhusiana na elimu wanayoitoa hasa katika upande wa usalama
barabarani. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo,
Profesa Zakaria Mganilwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa (katikati)
alipokua anatoa historia ya chuo hicho pamoja na kozi mbalimbali
zinazofundishwa katika chuo hicho, kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza
lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na
Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Naibu Mkuu wa
Chuo hicho kwa upande wa Taaluma Utafiti na Ushauri, Dk. Prosper Mgaya.
Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Usafirishaji wa Chuo cha Usafirishaji
nchini (NIT), kilichopo Mabibo, jijini Dar es Salaam, Amon Mwasandube,
akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
jinsi gari linavyokaguliwa linapokuja katika Kituo cha Ukaguzi wa Magari chuoni
hapo. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani
Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa
na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Mkuu wa
Chuo hicho, Profesa Zakaria Mganilwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment