Mwezeshaji
kutoka Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) Christopher Masaaka ambaye pia
ni Afisa Uchumi kutoka Halmashauri ya
Wangingómbe Mkoa wa Njombe akitoa mafunzo kwa moja ya kundi la washiriki wa
mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango,
Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Wagisha
Ronald na Hussein Kiranga (Katikati) kutoka Taasisi ya GIZ-TGPSH.
Baadhi
ya Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Manispaa ya Singida
wakijadili jambo wakati wa mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep)
iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za
Mitaa leo Mjini Dodoma.
Baadhi
ya Watumishi mbalimbali wakiwemo Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya
kutoka Halmashauri za Mkoa wa Manyara wakifuatilia mafunzo ya Mfumo wa
kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za
Mamlaka ya Serikali za Mitaa yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za
Umma (PS3) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani
(USAID) leo Mjini Dodoma.(PICHA NA
BEATRICE LYIMO-MAELEZO)
SHARE
No comments:
Post a Comment