TRA

TRA

Tuesday, August 29, 2017

Wasiwasi watanda visa vya ulaji wa nyama ya binadamu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Hofu imekumba kijiji cha Shayamoya katika jimbo la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini, baada ya kupatikana kwa maiti ya binadamu iliyonyofolewa myama yote.

Familia ya Zanele Hlatshwayo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ametoweka tangu mwezi Julai mwaka huu, ikiaminika kuwa ni mhasiriwa wa genge la watu wanaotuhumiwa kula nyama ya binadamu, ambapo tayari washukiwwa watano wamekamatwa.

Mwili wa mwanamke huyo ambo ulikuwa umeoza, ulipatikana baada ya mwanamume mmoja kudai kuwa mganga wa kienyeji, kuamua kujisalimisha kwa polisi juma lililopita, na kukiri kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
 Polisi walipata viungo kadhaa vya miili ya binadamu, wakati wa upekuzi kwenye nyu,mba moja ya mganga wa kienyeji
Polisi nchini Afrika kusiri awali walipuuza taarifa hiyo.
Waliamua kukubali taarifa hiyo baada ya mtu huyo kutoa mkono na mguu wa binadamu uliojaa damu kama ushahidi, hapo ndipo alipokamatwa mara moja na maafisa wa polisi.
Aliwaongoza hadi katika nyumba ya kukodishwa, ambapo polisi walipata masikio 8 ya binadamu, ndani ya chungu cha kupikia.
Inaaminika kuwa zingetumika kuwalisha wateja wakeambao wanaaambiwa yana nguvu za miujiza ya kumpa mtu pesa, nguvu na ulinzi wa kutosha.
Viungo vingine kadhaa vya mwili wa binadamu vilipatikana ndani ya mkoba.

Majabali

Maiti ya Bi Hlatshwayo uliojaa damu na mavazi yaliyokuwa yameraruka, ulipatikana miongoni mwa viungo vingine vya binadamu nyumbani mwa mganga huyo wa kienyeji.
Mavazi ya mwanadada huyo yalitambuliwa mara moja na jamaa zake.
Hata hivyo, polisi wangali wakisubiri matokeo ya uchunguzi wa DNA, ili kuthibitisha ikiwa mabaki ya maiti ni ya mwanamke huyo wa mvulana wa miaka miwili.
Familia ya Bi Hlatshwayo, bado haijamzika.
Mara nilipoingia kwwenye maskani ya Hlatshwayo, nilisalikumbana na nyimbo za huzuni na vilio kutoka kwa jamaa zake waliokuwa wakiomboleza
"Tunajaribu kuwaza tu namna alivyokuwa akiomba kutoumizwa au kuuwawa muda mfupi kabla ya kifo chake, alikufa kifo kibaya," alisema dadake mkubwa Nozipho Ntelele, huku akifuta machozi.
"Mavazi yake yalikuwa yamefunikwa kwa nyasi na vumbi, ambayo ni ishara tosha kuwa alipambana na wauwaji wake katika harakati za kunusuru maisha yake," aliongeza Bi Ntelele.

Harufu mbaya

Mganga huyo wa kienyeji anaishi katika nyumba moja ya kukodisha huko Rensburgdrift karibu na mji wa Estcourt.
Jina lake la utani ni "Mkhonyovu" inayomaanisha "Mtu mfisadi au tu mfisadi" katika lugha ya Ki-Zulu.
Amekodisha nyumba hiyo kutoka kwa Philani Magubane, ambaye kakake pia amekamatwa na maafisa wa polisi, kwa kuwa mshirika wa karibu wa mganga huyo wa kienyeji.
"Nilishtuka mno kubaini kuwa kakangu mdogo alimhusudu sana mganga huyo wa kienyeji huku akiamini hekaya zake- pale alipowaahidi utajiri, ilihali yeye alikuwa maskini hohe hahe tu kama mimi," Bwana Magubane aliniambia.
Anasema kuwa wateja wake mara kwa mara walikuwa wakilalamikia uvundo nyama iliyooza uliokuwa ukitoka katika nyumba ya mganga huyo wa kienyeji.

Wakaazi wakiri kula nyama ya binadamu

Mthembeni Majola, mwanasiasa wa eneo hilo, aliwakusanya wanakijiji kuhudhuria mkutano muda mfupi baada mshukiwa katika kisa hicho cha ulaji nyama ya binadamu kufikishwa mahakamanai kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.
Phepsile Maseko, ambaye ni mwanachama wa shirika la wanganga wa kienyeji, amelaani madai hayo ya ulaji wa nyama ya binadamu.
Anasema kuwa "Mkhonyovu" kwamba alikuwa mganga bandia ambaye alikuwa na tamaaa ya kutaka kujitajirisha binafsi na kufanya "matibabu yetu ya kienyeji kuchukiwa na kutoheshimiwa". 

CHANZO:BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger