
Majaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu.
KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania,
Prof. Ibrahim Khamis Juma mapema leo amewaongoza waombolezaji kutoa
heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Upendo Msuya aliyefariki dunia hivi karibuni.
Jeneza lenye mwili wa marehemu.
Prof.
Ibrahim amewaongoza baadhi ya majaji na viongozi wa kiserikali
waliofika nyumbani kwake, Tegeta jijini Dar ambapo pia baadhi ya
waombolezaji wamepata fursa ya kutoa heshima zao kanisani ilikofanyika
ibada fupi ya kumwombea marehemu.
Majaji wakipita kuaga mwili wa marehemu.
Baadhi
ya viongozi wa kiserikali walionekana kutoa heshima zao za mwisho
nyumbani hapo ni pamoja na Spika Msaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne,
Anne Makinda, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na wengine wengi
Majaji wakiendelea kuaga mwili wa marehemu.
Baba mzazi wa marehemu, akiaga mwili wa mwanaye.
Majaji wakiwa katika ibada ya kuaga mwili.
Mtoto wa kwanza wa marehemu Jaji Msuya akisoma wasifu wa mama yake.
Mume wa marehemu, Jaji Upendo Msuaya aitwaye Hilary Msuya (katikati) akiwa mwenye huzuni.
Watoto wa kike wa marehemu Jaji Msuya wakiomboleza.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Khamis Juma akitoa heshima za mwisho.
Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho.
Mbunge wa Kibamba Dar, John Mnyika akitoa heshima za mwisho.
SHARE



















No comments:
Post a Comment