TRA

TRA

Tuesday, September 5, 2017

Mambo ya Tigo na tiketi za Tigo Fiesta 2017

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa kutangaza ofa maalum za vifurushi zitazotolewa ununuapo tiketi ya tamasha la Tigo Fiesta kwa njia ya Tigo pesa. Pembeni ni Afisa Biashara wa Tigo, Edwin Mgoa

Tigo inatoa dakika 100 za muda wa maongezi, SMS  100 SMS na and 100 Mbs za data kwa manunuzi yote ya tiketi kupitia TigoPesa



Jumatatu 4 Septemba, 2017- Huku ikiwa imebakia siku chache tu kabla ya onesho la kwanza la msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa kufanyika jijini Arusha, wadhamini wakuu kampuni ya Tigo inazidi kutoa ofa kabambe kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za awali kupitia huduma ya TigoPesa.

Tigo inatoa dakika 100 za bure, SMS 100 za bure, na  kifurushi cha 100Mbs cha data bure kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zaoTigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa kupitia huduma ya TigoPesa.

Akitangaza ofa hiyo murwa jijini Dar es Salaam jana, Mkuu Mtendaji wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa ofa hii mpya ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za  data inaenda sambamba na ofa iliyopo sasa ya punguzo ya bei asilimia 10% kwa tiketi zote za awali za Tigo Fiesta 2017 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa au huduma ya kuhamisha fedha ya mitandao mingine yote ya simu nchini.

‘Kama tulivyoahidi hapo awali, tuna furaha kuthibitisha kuwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za ‘Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa’ kupitia Tigo Pesa, moja kwa moja watapata bonasi ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100 Mbs za data bure kutoka Tigo. Hii ni pamoja na ofa nono ya punguzo la 10% wanayopata wateja wote wa simu za mkononi wanaonunua tiketi zao za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya huduma ya kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao wa simu.’

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger