Na. Paschal Dotto- MAELEZO.
Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya rushwa katika ofisi
za Serikali, taasisi na mashirika ya umma na kuweka usawa katika
upatikanaji wa huduma kwa jamii.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John
Mbungo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kuhusu rushwa katika taasisi na
mashirika ya umma kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Brigedia
Jenerali Mbungo alisema kuwa lazima watumishi wajifunze kuwa waadilifu,
kwa hiyo kile watakachokipata kutoka katika mkutano huo kikafanye kazi
kuleta haki kwa wananchi wakati wa kupata huduma katika ofisi zao ili
kuendana na sera ya Awamu ya Tano ya kutokuvumilia vitendo vya rushwa
nchini.
“Tumieni
fursa katika kikao hiki ili kuweza kupata elimu itakayosaidia wananchi
kuelimika juu ya vitendo vya rushwa na kupata haki zao za msingi
wanapopata huduma katika ofisi zenu”,alisema Brigedia Jenerali Mbungo.
Kikao
kazi hiki ni cha kwanza ambacho kinafuatia mkakati wa awamu wa tatu
utakaokuwa wa miaka mitano kuanzia Julai, 2017 unaolenga kuanzia ngazi
za vijiji, wilaya, mkoa, mpaka taifa ili kudhibiti uadilifu, nidhamu na
utendaji kazi wenye kuzingatia haki katika ofisi mbalimbali nchini.
Aidha
Brigedia Mbungo alisema kuwa kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na
serikali, hali ya rushwa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa kwani
malalamiko yamepungua katika ofisi, taasisi na mashirika ya umma.
“Hali
ya rushwa sasa hivi imepungua kwa sababu Serikali kwa kutumia juhudi
mbalimbali imedhibiti hali hii, Tanzania ina viwango vya chini sana vya
rushwa ikilinganishwa na nchi nyingine za maziwa makuu kwa hiyo naweza
kusema kiwango kimepungua sana hususani kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo
vitendo hivi vilishamiri sana, hivyo katika awamu hii ya tatu ya
mkakati huu tunatarajia viwango vitashuka zaidi”, alisisitiza Brigedia
Jenerali Mbungo.
Naye
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Theresia Mmbando alisema kuwa
katika mkoa wa Dar es Salaam hali ya vitendo vya rushwa imepungua kwa
kiasi kikubwa na sasa wananchi wanapata huduma pasipo kuwa na dalili
zozote za rushwa.
“Hali
ya rushwa katika mkoa wetu wa Dar es Salaam inapungua siku hadi siku
kwa kuwa watu wanaendelea kupata elimu ya haki zao za msingi na
kuhudumiwa pasipo kutoa rushwa, wala kuwepo dalili za rushwa”, alisema
Bi. Mbando.
Kwa
upande wake Mkuu wa TAKUKURU, kanda maalum ya Dar es Salaam
Bw.Juventus Baitu ameeleza kuwa wamefanikiwa kuweka sawa mkakati huo
kwa kutoa elimu kwa wananchi na kwa sasa kumekuwa na mwamko wa kuripoti
matukio ya rushwa katika ofisi yake.
Aliongeza
kusema kuwa katika kitengo cha Dawati la Uchunguzi wamepokea malalamiko
yapatayo 665 kwa mkoa wa Dar es Salaam huku kitengo hicho kikifungua
majalada ya kesi 40 kwa Mwendesha Mashtaka (DPP) na kusikilizwa kesi 26
ambapo taasisi hiyo ilifanikiwa kushinda kesi 14 na kuokoa kiasi cha
pesa kisichopungua shilingi milioni 791,443,984 katika kesi mbalimbali
za rushwa.
Aidha
TAKUKURU kupitia dawati la elimu ya rushwa imeweza kufungua vilabu 94
vipya katika shule mbalimbali mkoani Dar es Salaam, kuendesha semina 91
kwa watumishi wa taasisi na mashirika ya umma pamoja na maonesho 12
yanayohusu vitendo vya rushwa ikiwemo kuwahabarisha wananchi kupitia
vipindi vya televisheni 14 kuanzia mwaka 2016 pamoja na kutoa taarifa
kwenye vyombo vya habari kwa kutoa vitini 19 kuhusu mapambano dhidi ya
rushwa.
“Tumeweza
kutoa elimu kupitia matamasha mbalimbali zaidi ya 16 katika taasisi na
mashirika ya umma ambapo matamasha 7 yalikuwa na lengo la kutoa mazimio
kwa taasisi na mashirika ya umma kuhusu kwa vitendo vya
rushwa”,alisisitiza Bw.Baitu.Mkakati
huo kwa awamu ya tatu ulizinduliwa rasmi, Desemba 10, 2016 wakati wa
maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu duniani na Makamu wa
Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo utekelezaji wake ulianza tarehe
1, Julai, 2017.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao
kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa
mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) jana jijini
Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Bibi. Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bw. Edward
Mpogolo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bibi. Theresia Mmbando akielezea
jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za
kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya
rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Kitengo cha Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Bi. Christina Maganga
akitoa neno la utangulizi kuhusu mkakati wa taifa dhidi ya rushwa awamu
ya tatu wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati za
kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati huo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya kudhibiti uadilifu kutoka mkoa wa Dar es Salaam
wakifuatilia wakifuatila mada wakati wa kikao kazi cha wajumbe wa
kamati hizo kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa,
awamu ya tatu (2017-20120) jijini Dar es Salaam.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Brigedia Jenerali John Mbungo akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu
mkakati wa taifa dhidi ya rushwa toka kwa Mratibu wa Kitengo cha Utawala
Bora Ofisi ya Rais, Bi. Christina Maganga (hayupo pichani) wakati wa
hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti
uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Bibi. Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya
Ilala Bw. Edward Mpogolo.
Mkuu
wa Takukuru Kanda Maalum ya Dar es Salaam Juventus M. Baitu
akiwasilisha mada kuhusu hali ya rushwa katika mkoa wa Dar es Salaam
wakati wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu
utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu
(2017-20120).
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Brigedia Jenerali John Mbungo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
washiriki wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu
kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu
(2017-20120) jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija- MAELEZO
SHARE
No comments:
Post a Comment