TRA

TRA

Thursday, September 7, 2017

TUNDU LISSU AVAMIWA NA KUPIGWA RISASI NYUMBANI KWAKE MKOANI DODOMA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.
Chanzo: Mwananchi

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger