TRA

TRA

Monday, October 2, 2017

Kolabo ya Izzo Business na Avril gumzo kubwa Coke studio

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wanaendelea kupata burudani ya muziki kutoka kwa wasanii nguli kutoka nchi za Afrika kupitia onyesho la Coke Studio linalorushwa na Clouds TV ambapo mwishoni mwa wiki ‘kolabo’ ya mwanamuziki kutoka nchini, Izzo Business na Avril kutoka Kenya imeacha gumzo kubwa.
Wanamuziki wengine waliopagawisha mashabiki wa muziki katika onyesho hilo ni  Mafizikolo kutoka Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na msanii Nyashinski kutoka nchini Kenya na wasanii waalikwa Bill Nas (Tanzania), Sheebab (Uganda) na Asgeg Ashko (Ethiopia).
Akiongea juu ya kolabo hii, Izzo Business alisema amefurahi kushirikiana na Avril kimuziki hususani wimbo walioimba pamoja unaojulikana kama ‘kanyonyi kanja’ na ‘mabata mabata  yanaogelea’ ambao umeimbwa kwa lugha ya Kiswahili ukiwa na vionjo vya muziki wa bongofleva.
Kupitia onyesho hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni ya Coca-Cola, muziki wa Tanzania unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya wanamuziki kutoka hapa nchini ambao wanashirikiana na wenzao kutoka Afrika. Shindano hili linarushwa kwenye luninga kwenye nchi zaidi ya 50.
Wasanii wa Tanzania waliopo katika onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness, Nandy na mtayarishaji nguli wa muziki wa studio, Nahreel.
Wakitoa maoni yao kuhusiana na onyesho hili, baadhi ya wapenzi wa muziki kutoka mikoa mbalimbali wanaolifuatilia walisema kuwa burudani za Coke Studio msimu huu ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa kolabo za wanamuziki zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba zikionyeshwa zinaleta furaha na kumfanya mtazamaji kujiona anaangalia onyesho la wanamuziki hao mubashara (Live).
Mbali na wasanii wa Tanzania,wasanii msimu huu wa tano wa Coke Studio unawajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda,  Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Cameroon.
Baadhi ya wasanii hao ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya), Sami Dan  (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda ( Uganda).
Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana.
Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger