Mkurugenzi wa Kampuni Msama
Auction Mart , Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika
ofisi za Kampuni hiyo Kinondoni Moroco jama wakati akipmogeza Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa hatua mbalimbali anazochukua
kulinda kazi za wasanii zisiibiwa.
Mkurugenzi wa Kampuni Msama Auction Mart , Alex Msama akifafania jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumza nao.
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii wakichukua matukio katika mkutano huo.
………………………………………………………………………….
Kampuni ya Msama Auction Mart
imempongeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe kwa kauli yake kuhusu wizi wa kazi za sanaa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema
kuwa Kampuni yao imeona kuwa Waziri huyo ameonesha nia yakupoteza kabisa
kazi feki za Sanaa.
Hatua hiyo ya Waziri pia
itawagusa wenye kazi zao ambao ni Wasanii wa kazi hizo ikiwemo Wasanii
wa Bongo Fleva, Nyimbo za Injili, Maigizo na Filamu.
Msama amesema kuwa doria za
kumaliza wizi huo wa kazi za Wasanii inaendelea kwa nchi nzima, ambapo
Mkoa mmoja tu ndiyo wenye ahueni yakupunguza wizi huo ambao ni Mwanza.
“Msama Auction Mart kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo inategemea kuanza zoezi lakumaliza kazi feki za sanaa nchini,
zoezi ambalo lisilokuwa na mwisho”, amesema Msama.
Pia Msama ameonya wale wote
wanaofanya biashara za kuuza kazi feki, ambapo amesema kuwa
watakapokamata Kompyuta za kufanyia kazi hizo basi hazitarudi tena kwa
wahusika.
Wafanyabiashara wa Filamu za Nje
nao wametakiwa kuacha kufanya biashara hizo bila kibali cha mwenye kazi
husika, kwani hatua hiyo inaikosesha Serikali mapato.
SHARE
No comments:
Post a Comment