Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Ofisi ya walimu iliyojengwa
kisasa katika shule ya msingi Kwala wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiipongeza kamati ya ujenzi kijiji cha Kwala
wilayani Kisarawe kwa ujenzi wa madarasa mapya.
Baashi ya matundu ya vyoo yaliyokamilika kujengwa wilayani Kisarawe.
Diwani wa kata ya Mzenga Mohamed
Lubondo(katikati) akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani
Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya
msingi Mitengwe wilayani Kisarawe.
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Mitengwe wilayani Kisarawe.
………………….
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye
pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo
amewapongeza wananchi wa kisarawe kwa ushirikiano mkubwa katika ujenzi
wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, Ofisi za walimu,
nyumba, pamoja na vyoo.
Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa
akikagua mradi ya ujenzi wa madarasa wilayani kisarawe katika vijiji
vya Mitengwe, Kitonga, Boga, na kwala.
Katika vijiji hivyo, Jafo alikagua
ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 15, Ofisi za walimu 4, pamoja na
matundu ya vyoo 40 ambapo ujenzi wake unafanyika kwa bora unaotakiwa.
Kutokana na mwamko mkubwa
ulioonyeshwa na wananchi hao katika kushirikiana na serikali na viongozi
walio wachagua akiwemo mbunge na madiwani wote wa kisarawe, Jafo
amesisitiza wananchi wengine katika wilaya mbalimbali kushirikiana na
serikali pamoja na viongozi wao ili kujiletea maendeleo.
SHARE
No comments:
Post a Comment