TRA

TRA

Wednesday, October 4, 2017

TAASISI ZINAZONYANYASA WANAWAKE KUKIONA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Na Venance Matinya, Mbeya

SERIKALI imeahidi kufanya utafiti ili kubainia Taasisi za Elimu ambazo bado zinaendeleza Unyanyasaji wa Kijinsia kwa wanawake na kuchukua hatua stahiki zitakazotoa fundisho kwa maeneo mengine.

Naibu Spika Dk Tulia Ackson alitoa ahadi hiyo alipofungua Mkutano wa nne wa Kamati ya Wanawake Taifa ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu nchini(THTU) uliofanyika jijini Mbeya.

Dk Tulia alisema Serikali imekuwa ikifanya kila juhudi kuhakikisha unyanyasaji wa kijinsia unakomeshwa katika Taasisi za Elimu lakini kwakuwa bado kuna malalamiko ipo haja ya kufanyika kwa utafiti ili kubaini maeneo ambayo yanaendeleza tabia hiyo.

Alisema hakuna mwanamke aliye mwanafunzi au mfanyakazi anayetakiwa kuendelea kunyanyasika kwa kwa kulazimishwa kufanya mapenzi ili aweze kufaulu au kupanda cheo na popote palipo na mazingira hayo ni lazima pafanyiwe kazi ili kurekebisha.

Hata hivyo Dk Tulia amewasihi watumishi na wanafunzi wa kike kutambua kuwa wao ndiyo walio na maamuzi ya kukataa unyanyasaji wa namna hiyo kwa kuweka misimamo yenye kulenga kulinda heshima na utu wao ndani ya jamii.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Wanawake Taifa ya THTU, Amina Mdidi alizitaja changamoto zinazoendelea kuwakabili wafanyakazi wanawake kwenye taasisi za Elimu ya juu kuwa ni pamoja na Uhaba wa vitendea kazi,mazingira yasiyo rafiki na ongezeko la makato kwenye mishahara.

Ameshauri pia Serikali kupitia upyaa mitaala ya masomo kuanzia shule za msingi ili kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa Nadharia na vitendo hatua aliyosema itawajengea uwezo wanafunzi wa kujiajiri kupitia ujasiriamali na pia uzalendo kwa Taifa lao.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa THTU,Dk Emeria Mgonzibwa alisema Sera ya Viwanda inayoendelea kupiganiwa na Rais Dk John Magufuli na Waziri wa Viwanda Charles Mwijage itawezekana pale Taasisi za Elimu ya juu zitakapotoa wahitimu walio na ujuzi wa kutosha na wanaoweza kuajiriwa na kujiajiri.

Mwisho.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger