Na Hamza Temba – WMU
…………………………………………………………..
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amepokea taarifa ya utekelezaji
wa agizo alilotoa la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori MBOMIPA na kuagiza rasimu hiyo ifanyiwe marekebisho ya mwisho
kabla ya kuwasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya mijadala na hatua zaidi za
kukamilisha rasimu hiyo.

Alipokea
taarifa hiyo juzi (Ijumaa, Septemba 29, 2017) katika kikao alichokiitisha
kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mjini Iringa. Aliagiza
kuundwa upya katiba hiyo alipofanya ziara ya kikazi kwenye eneo la Jumuiya hiyo
katika kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa mapema mwezi Agosti mwaka huu.

Kufuatia
ziara hiyo pamoja na taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza suala hilo alibaini
mapungufu mbalimbali ya kikatiba na kuamua kutoa agizo la kuundwa upya kwa katiba
hiyo na kuvunja kabisa bodi ya wadhamini
ya jumuiya hiyo. Miongoni mwa mapungufu hayo ni katiba iliyokuwepo awali
kukinzana na Sheria mama pamoja na kanuni zake.

Katiba
kutoeleza namna ya upatikanaji wa viongozi na namna ya kuwawajibisha, kutoeleza
majukumu ya bodi ya wadhamini kwa usahihi na namna ya upatikanaji wa bodi hiyo
pamoja na kutoleza wajibu wa wawekezaji katika jumuiya kwa jumuiya yenyewe na
kwa Serikali kwa ujumla wake.

Kubwa
zaidi ambalo lilisababisha kuvunjwa kwa bodi hiyo ni jumuiya hiyo kujiendesha
kwa hasara huku ikiomba fedha kwa wahisani kwa ajili ya kujiendesha wakati
kimsingi asasi hiyo ilipaswa kuwa msaada mkubwa kwa wanachama wao ambao ni
vijiji vinavyounda Jumuiya hiyo.

Taarifa
ya utekelezaji wa agizo hilo iliwasilishwa kwenye kikao hicho na Mwanasheria wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Kissah Mbilla kwa niaba ya Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo. Taarifa hiyo ilijadiliwa na kutolewa mapendekezo mbalimbali
ya kuiboresha.

“Baada
ya michango yote hii mizuri tuliyotoa hapa leo, nendeni sasa mkairekebishe
vizuri izingatie maeneo yote ya msingi ikiwemo mgawanyo sawa wa mapato, kuzingatiwa
kwa maeneo ya mapito ya wanyamapori na idadi ya wanachama ijumuishe vijiji
vyote vilivyoanzisha Jumuiya hiyo ili kuepusha migogoro ya baadaye inayoweza
kujitokeza” aliagiza Prof. Maghembe.

Kikao
hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo
Makani ambaye ni alikuwa Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Waziri Maghembe
kuchunguza mgogoro huo wa MBOMIPA, baadhi ya wajumbe wa tume hiyo na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Amina
Masenza.

Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA iliundwa mwaka 2007 ikiwa wanachama ambao ni
vijiji 21 vilivyopo katika tarafa ya Idodi na Pagawa kwenye halmashauri ya
Wilaya ya Iringa Vijini mkoani Iringa. Eneo la jumuiya lina ukubwa wa kilomita
za mraba 777 na linapakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Eneo
hilo limekuwa likitumika kwa ajili ya shughuli za utalii wa picha, utalii wa
uwindaji, utalii wa kiutamaduni na utalii wa kutembea kuangaliwa wanyama.
Miongoni mwanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni ndege wa aina
mbalimbali, mamba, tembo, nyati, swala na wengineo wengi ambao huingia na
kutoka kutokea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati)
akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo
baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti
mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori
MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo,
Mhandisi Ramo Makani na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia)
akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakati wakiagana baada ya
kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu
la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na
kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo mkoani Iringa jana. Nyuma yake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo,
Mhandisi Ramo Makani na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia)
akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo
baada ya Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) kupokea
taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la
kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na
kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo
baada ya Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) kupokea
taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la
kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na
kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia)
akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo
baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti
mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori
MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akichangia hoja ya kuboresha rasimu ya katika mpya ya MBOMIPA katika kikao hicho.
Mwanasheria
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Kissah Mbilla akiwasilisha taarifa
hiyo mbele ya Waziri Maghembe na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Iringa.
SHARE
No comments:
Post a Comment