Kila
tarehe Moja ya Mwezi Oktoba (Oktoba Mosi) ni siku ambayo dunia nzima
huadhimisha siku ya Wazee kwa lengo la kuwatambua na kuwaenzi wazee.
Mkoa wa
Shinyanga umeadhimisha siku hii muhimu leo Oktoba 1,2017 katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga,Zainab Telack.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuelekea uchumi wa viwanda;Tuthamini mchango,uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa”.
Akihutubia
katika maadhimisho hayo,Matiro alisema serikali inatambua umri wa mzee
ni kuanzia miaka 60 na kuendelea na kwamba kila mmoja anapaswa kutambua
kuwa siku moja ataufikia uzee hivyo wazee wanapaswa waheshimiwe,watunzwe
na kuenziwa.
“Nawasihi
tutumie hekima na ushauri walionao wazee wetu na siyo kuanza kuwafanyia
vitendo vya ukatili kwa kuwanyanyasa,kuwatenga na kuwaua kwa imani
potofu,na serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa
watakaonyanyasa wazee kwa namna yoyote ile”,alisema Matiro.
Katika
hatua nyingine aliziagiza halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga ambazo
hazijatekeleza zoezi la kutambua wazee na kuwapatia kadi za matibabu
bila malipo.
“Mkoa
wetu una wazee 59,871 waliotambuliwa,kati yao waliopata kadi za matibabu
bila malipo ni 7,553,waliopatiwa kadi z za mfuko wa afya ya jamii ni
4,613,bado idadi ni ndogo..Nawaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha kuwa
kila mzee aliyetambuliwa anapata kadi ya matibabu bila malipo kabla ya
tarehe 30.10.2017”,alieleza Matiro akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa.
Aidha
aliwahakikishia wazee kuwa mkoa wa Shinyanga utaendelea kuhakikisha kuwa
dawa zote za magonjwa ya wazee zinapatika kwenye vituo afya huku
akiwataka wakurugenzi wa halmashauri kufanya ukaguzi wa dawa na fedha
kwa kila robo ya mwaka.
Alitoa
rai kwa uongozi wa idara za afya kuanzia ngazi ya mkoa kuhakikisha kuwa
uwepo wa vyumba maalum vya kutolea huduma za afya kwa wazee na kuwapa
kipaumbele na kuweka ujumbe wa “Mpishe Mzee Apate Huduma Kwanza”.
“Kuelekea
uchumi wa viwanda;Tuthamini mchango,uzoefu na ushiriki wa wazee kwa
maendeleo ya taifa,kila mmoja atimize wajibu wake ili wazee wetu wapate
huduma bora katika nyanja zote”,aliongeza.
Akisoma
risala,Katibu mkuu wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa
Shinyanga,Underson Lyimo aliomba changomoto zinazowakumba wazee
zishughulikiwe ili wazee waishi kwa amani na usalama.
“Bado
wazee hawaheshimiki,wanatengwa na kunyanyaswa na hata kuuawa,tunaomba
tabia hizi zikomeshwe,hatua stahiki ziendelee kuchukuliwa kwa wanaokiuka
haki za binadamu na elimu itolewe kwa jamii kuhusu sera ya taifa ya
wazee,haki na wajibu wa kuwalinda wazee”,alisema Lyimo.
Maadhimisho
ya siku ya wazee duniani mkoa wa Shinyanga yameenda sambamba na zoezi
la kugawa kadi za matibabu bure kwa wazee 7,553.
Pia
kumefanyika zoezi la upimaji afya kwa wazee wote pamoja na wananchi
wengine ambapo washiriki wa maadhimisho hayo wamepima bure magonjwa
yasiyoambukiza kama kisukari,shinikizo la damu,magonjwa ya macho na
mengineyo.
TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho ya
siku ya wazee duniani mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga,Zainab Telack.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la
Wazee mkoa wa Shinyanga, Faustine Masale Sengerema,kushoto ni Katibu
mkuu wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga,Underson Lyimo.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alitumia fursa hiyo kuwaomba wazee
kushiriki katika kampeni ya upandaji miti inayoendelea mkoani Shinyanga.
Wazee wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya wazee.
Aliyesimama
ni Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Alfred Shayo akizungumza
katika maadhimisho hayo ya siku ya wazee ambapo alisema ‘Wazee ni hazina
na uzee ni dawa hivyo jamii inategemea ushauri wa wazee ili kujenga
taifa”.
Wazee wakiwa katika maadhimisho hayo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga, Faustine Masale
Sengerema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wazee ambapo alisema
wazee wanaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli katika
kuwaletea maendeleo wananchi.
Wazee wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea….
Katibu
mkuu wa Baraza la Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga,Underson Lyimo
akisoma risala ambapo alizipongeza halmashauri zilizofanikisha zoezi la
kutoa kadi za matibabu bila malipo kwa wazee zikiongozwa na halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga.Aliyeshikilia kipaza sauti ni Afisa Maendeleo ya
Jamii Sekretarieti ya mkoa wa Shinyanga Glory Mbia.
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume,Mwenyekiti wa Baraza la
Ushauri la Wazee mkoa wa Shinyanga, Faustine Masale SengeremaMkuu wa
wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakifuatilia risala.
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumzia kuhusu
upatikanaji wa dawa mkoani humo.Alisema suala la changamoto ya dawa
limepungua kutokana na vituo vya afya kuwa na fedha za kutosha za
kununulia dawa na vifaa tiba.
Madaktari wakiwa katika eneo la tukio
Afisa
ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga,Lydia Kwezigabo akielezea kuhusu zoezi
la kutambua wazee katika mkoa wa Shinyanga ambapo alisema jumla ya
wazee 59,871 wametambuliwa na kati yao 7,553 sawa na asilimia 12.8
wamewakabidhi kadi za matibabu bila malipo na kuitaji wilaya ya
Shinyanga kuwa ndiyo yenye idadi kubwa ya wazee waliopatiwa kadi
hizo.Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Sekretarieti ya mkoa wa Shinyanga Glory Mbia.
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akionesha moja ya kadi za
matibabu bila malipo zilizoandaliwa kwa ajili ya kuwapatia wazee
waliotambuliwa.
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi kadi ya matibabu bila
malipo kwa mzee Faustine Masale Sengerema ambaye ni miongoni mwa wazee
7,553 wanaopatiwa kadi hizo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi kadi ya matibabu bila malipo kwa mzee Philipo Njabuga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi kadi ya matibabu bila malipo kwa Bi. Sayi Zengo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi kadi ya matibabu bila malipo kwa Bi. Suzana Shija.
Wataalam wa afya wakiwa katika eneo la tukio.
Wazee wakiteta jambo wakati wa zoezi la upimaji afya kwa magonjwa yasiyoambukiza.
Mtaalam akimpima macho mmoja wa wazee waliojitokeza kupima afya zao.
Zoezi la upimaji afya likiendelea
Vijana wa Compassion wakiimba wimbo kuhusu “Amani”
Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment