Rais wa zamani wa
Marekani Barack Obama alifika katika majengo ya mahakama moja Chicago
kuitikia wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza la mahakama.
Obama akipokea salamu kutoka kwa watu waliofika kumuona
Hata hivyo, jaji alimwamuru aondoke bila kuhudumu.Umati wa watu ulikusanyika katika jengo la manispaa la Daley Center kumuona rais huyo wa 44 wa Marekani, ambaye ana nyumba katika jiji la Illinois.
Bw Obama aliondoka kwake nyumbani mwendo wa saa tatu unusu saa za huko siku ya Jumatano na aliondoka majengo ya mahakama saa sita hivi mchana.
Kila mtu aliyekabidhiwa wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza mahakamani hupokea hundi ya $17.20 (£13.11) kutoka kwa wilaya hiyo.
SHARE









No comments:
Post a Comment