Rais John Magufuli ameanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini Uganda kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni.
Dk Magufuli aliyeongozana na mkewe
Janeth amewasili Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda ambako amepokewa
na mwenyeji wake Rais Museveni aliyeambatana na mkewe Janeth.
Katika mapokezi hayo leo Alhamisi
Novemba 9,2017, Rais Magufuli amepigiwa mizinga 21 na amekagua gwaride
lililoandaliwa kwa heshima yake.
Wakiwa mpakani, viongozi hao wawili
watafungua kituo cha pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post -
OSBP) kilichojengwa ili kurahisisha utaratibu wa forodha, uhamiaji na
kuharakisha biashara kati ya nchini hizi mbili.
Taarifa ya Ikulu imesema baadaye leo,
marais hao wataweka jiwe la msingi katika mradi wa bomba la mafuta ghafi
linaloanzia Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Shughuli hiyo itafanyika katika Kijiji cha Luzinga, kilichopo mkoani Rakai nchini Uganda.
Baada ya ufunguzi, viongozi hao
watazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika
wilayani Kyotera nchini Uganda.
Rais Magufuli jioni ya leo atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais Museveni katika mji wa Masaka.

SHARE









No comments:
Post a Comment