TRA

TRA

Thursday, November 9, 2017

UVCCM WILAYA YA GEITA YAVUNA VIJANA 50 WA CHADEMA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 
Katibu wa UVCCM wilaya ya Geita Ally Rajabu akiongozana na baadhi ya vijana wakati wa zoezi la kuweka bendera za chama hicho kwa mabarozi wa kijiji cha Buligi kata ya senga ambapo kunatarajia kufanyika uchaguzi hivi karibu wa kiti cha Diwani.

Vijana wa UVCCM wakisimika bendera ya chama cha mapinduzi.

Katibu wa UVCCM Wilayani Geita pamoja na vijana wakikimbia wakati wa zoezi la kuweka bendera.

Vijana wa UVCCM wakisimika bendera ya chama cha mapinduzi.

Katibu wa UVCCM,Ally Rajabu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama pamoja na mabalozi wa mashina.



PICHA NA JOEL MADUKA
Vijana  hamsini (50 )wa chama cha demokrasia na
maendeleo( CHADEMA )wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi(
CCM) katika kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wakati wa uzinduzi
wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa
chama hicho, (UVCCM).
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo ulioambatana na zoezi la kusimika bendera kwamabalozi,
Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw Ali Rajab alisema  vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM
kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Dr John Magufuli.
Bw Rajab pia
amewataka pia ameongeza kwa kuwataka  watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili
kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ujumla.
Katibu wa
Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi Mazoea Salim, amesema
wanatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga .

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger