TRA

TRA

Wednesday, December 6, 2017

MHANDISI KAMWELWE ATEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA MFUMO WA UZALISHAJI NA UGAWAJI MAJI CHALINZE UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI KUPITIA DAWASA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI
WA Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe ametembelea na
kukagua maendeleo
ya ujenzi Mradi wa maji awamu ya tatu ya upanuzi wa chanzo na mtandao wa maji
wa Chalinze mkoani Pwani leo Desemba 6, 2017.

Mradi
huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi
na Maji Taka, (DAWASA), upanuzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa matenki na
ulazaji wa mabomba, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji pamoja na ujenzi wa Ofisi
mpya za Mradi.
“Mradi
huu unahusisha  upanuzi wa mtambo wa
kusafishia maji wa Chalinze ambao chanzo chake ni Mto Wami na lengo ni kuongeza
uzalishaji kufikia mita za ujazo Elfu Tisa (9000) kwa saa kutoka mita za ujazo
Mia Tano (500) kwa saa.” Amefafanua Mhandisi Kamwelwe.
Akifafanua
zaidi Mhandisi Kamwelwe amesema, Mradi pia unahusisha ujenzi wa
Matrenki 19, ulazaji
wa mabomba ya ukubwa tofauti wenye urefu wa kilomita 1,022, ujenzi wa vizimba
vya kuchotea maji 351 katika  vijiji na
vitongoji vya Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo Mkoani Pwani.
“Mradi
huu ni Mkubwa na unahusisha pia baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga na Morogoro
katika wilaya za Handeni na Ngerengere.” Ameongeza Waziri huyo.
Aidha
Mheshimiwa Waziri, alisema Wananchi wa maeneo yatakayofaidika na Mradi huo
ambao ni Mkubwa ni pamoja na wakazi wa Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga,
mji na vitongoji vya Chalinze, na baadhio ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha Mkoani
Pwani, wakazi wa maeneo ya Kizuka A na B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi
Bwawani  pamoja na Sangasanga A
na B Mkoani
Morogoro.
Maeneo
mengine yatakayojengwa matenki ni pamoja na Pera, Pingo, Bwilingu, Msoga,
Diozile, Lugoba, Mindutulieni, Saleni, Mazizi, Msata, Kihangaiko, Kilemera,
Hondogo, Miono North 3, Kimange, Rupungwi na Manga.
Kati
ya matenki hayo 19 mojawapo ni tenki kuu la Mazizi lenye uwezo wa kuhifadhi
lita Milioni 2, kukamilika kwa ujenzi wa tenki hiulo kutafanya kuwa tenki kubwa
zaidi kuliko yote Mkoani Pwani.
Kwa
mujibu wa Mhandisi Kmwelwe, Mradi utrakapokamilika utagharimu dola za
KImarekani Milioni 41.36 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya
India kupitia Benki ya Exim yta nchini humo. Hata hivyo Waziri
ameonyesha kukerwa kwake na kusuasua kwa mkandarasi kumalizia kazi
hiyo kwa muda uliopangwa na kwamba kama asingefuata ushauri wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Wataalamu wa Wizara yake, basi leo Desemba
6, 2017 ilikuwa siku ya kuvunja mkataba wa Mkandarasi huyo. “Hata
hivyo Mkandarasi baada ya kuahidi kukamilisha mradi Februari 8, 2017,
tumeona tumuache hadi muda huo, lakini akishindwa hatuna njia nyingine
ni kuvunja mkataba na kutafuta Mkandarasi mwingine.” Alionya Waziri
Kamwele wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye chanzo cha
maji Mto Wami.
Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete,
amemshukuru Waziri Kamwele na Serikali ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, kwa nia yake ya dhati ya kuwaondolea kero ya maji wakazi wa
Chalinze, na kwamba ana imani kubwa ya kukamilika kwa mradi huo baada
ya kuulalamikia kwa muda mrefu bungeni kuwa umechelewa sana.
“Mheshimiwa Waziri napenda nikushukuru sana na hasa Mheshimiwa Rais
wetu Mpendwa Dkt. John Magufuli, kwa kazi nzuri ambayo Serikali
inafanya katika kutatua kero za wananchi na hasa wapiga kura wa jimbo
la Chalinze.” Alisema Mhe. Kikwete.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack
Kamwelwe, (wane kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Majid Mwanga, Watatu
kulia, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, (watatu
kushoto),Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang’ingo, (wapili
kulia), Mkandarasi wa Mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji kutoka
kampuni ya WAPCOS Limited ya India, Mhandisi  P.G. Rajani na
maafisa wengine, wamiwa mbele ya tenki la kusafishia maji linalojengwa
chini ya mradi huo unaoendeshwa na Sewrikali kupitia DAWASA, kwenye
chanzo cha Maji Mto Wami, Mkoa wa Pwani, Desemba 6,
2017

Mhe. Mhandisi Kamwelwe, akizungumza jambo na Mhe. Ridhiwani
Kikwete, walipotembelea chanzo cha Maji Mto Wami.

Mbunge wa Bagamoyo, Mhandisi, Dkt.Shukuru Kawambwa, akimsikiliza
Mhe. Waziri Kamwelwe, wakati wa ziara ya Waziri wilayani Bagamoyo
kukagua ujenzi wa tenki la kuhifadhia Maji, Desemba 6, 2017. Tenkji
hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 6.

Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang’ingo, akitumia
mchoro kuelezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tenki la Maji Bagamoyo
Mkoani Pwani, Desemba 6, 2017

Mhe.Waziri Kamwelwe, akisalimiana na mmoja wa mafundi wanaojenga
tenki la kuhifadhia maji Bagamoyo.

Mkandarasi wa Mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji kutoka
kampuni ya WAPCOS Limited ya India, Mhandisi  P.G. Rajani,
akitumia mchoro kumueleza Waziri Kamwelwe, (wapili kuhsoto) na
Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang’ingo, kuhusu maendeleo ya
ujenzi wa mradi huo

Taswira ya ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lita milioni 6,
Bagamoyo Mkoani Pwani kama inavyoonekana Desemba 6, 2017

Mhbe., Kamwelwe, (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Majid
Mwanga, (wapiili kulia) na Wakandarasi kutoka kampuni ya India ya
WAPCOS.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger