TRA

TRA

Wednesday, December 27, 2017

SEKRETARIET YA MAADILI YAHIMIZA VIONGOZI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


umi1
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipowawataka Viongozi wote wa umma nchini  kuorodhesha mali zao  kisha kukabidhi kwa Sekretarieti kabla ya Desemba 31 mwaka huu Kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo Bw. Filotheus Manula.
umi2
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katikati  akikaribishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Rodney Thadeus ili kuzungumza na waandishi wa habari,  wa pili kutoka kulia ni Aisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Filotheus Manula na kushoto ni Ofisa wa Sekretarieti hiyo Bw. Waziri Kipacha
………………………………………………………………………….
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewahimiza  Viongozi wote wa umma nchini  kuorodhesha mali zao  kisha kukabidhi kwa Sekretarieti kabla ya Desemba 31 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo amesema  kufanya hivyo ni utaratibu ambao upo kwa mujibu wa sheria ,hivyo lazima watekeleze kwa wakati na watakaoshindwa hatua za kinidhamu  zitachukuliwa dhidi yao.
, Jaji Mstaafu  Nsekela ameongeza kwamba mwisho kwa viongozi wa umma kukabidhi tamko la mali zao na kufafanua  kuwa viongozi wanaotakiwa kuorodhesha mali zao na kisha kukabidhi Sekretarieti ya Maadili ni wale wa kuteuliwa na kuchaguliwa.
“Kila kiongozi wa umma ajaze tamko hilo kwa kuorodhesha mali zake, mwenza wake na watoto wake walio na umri chini ya miaka 18,”amesema.
Ameongeza kuwa viongozi ambao wanastaafu wakati wanaingia waliorodhesha mali zao, hivyo wanapostaafu ni lazima waoredheshe ili ifahamike wanatoka wakiwa na mali kiasi gani.
Ili kufikia malengo ya  tamko hilo kisheria linalowahusisha pia viongozi waliostaafu na wale wanaoelekea kustaafu, Ameongeza kwamba Fomu za tamko zipo kwenye tovuti ya sekretarieti ya maadili.
Amesema anaamini viongozi wanafahamu wajibu wao,hivyo wafanye haraka  iwezekanavyo na hasa kwa kuzingatia muda uliobakia ni mchache.
Kuhusu viongozi wanaostaafu ambao wamejaza tamko hilo amesema nao bado lakini katika eneo hilo kuna changamoto yake kidogo kwani viongozi wanapostaafu inakuwa ngumu kuwapata lakini nao watambue wanatakiwa kujaza tamko kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Ofisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti  ya maadili Bw. Filotheus Manula ameongeza kuwa ujazaji wa tamko la mali kwa viongozi wa umma ni takwa la kikatiba na kuna adhabu kwa wasiofuata.
Ametaja adhabu hizo ni kuonywa, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na wakati mwingine kufukuzwa kazi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger