Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye
maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama
yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja
kutumia madarasa hayo na kujenga madarasa bora.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais
Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga
uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.
“Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na
Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka
leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora
watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi
nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe
yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi watajiskia fahari
kusoma”Alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi kuhusu Usimamizi wa Ujenzi
wa Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika
ameneo yote yote Nchini.
Niwapongeze baadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri
sana ya Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha
ujenzi na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo
hivyo na nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea
Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.
Waziri Jafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo
mafunzo haya kuheshimu mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini,
kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.
Awali akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa mafunzo haya
yanakamilisha mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa K. Majaliwa miezi nane
iliyopita na baada ya mafunzo haya yanayoanza leo tutakuwa tumewafikia
Viongozi 324.
Prof.Semboja aliongeza kuwa Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo
ambayo yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni
kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi wa Kimkakati kwa kuzingatia
mahitaji ya jamii kwa manufaa mapana ya sasa nay a baade ya Jamii
Tunayoihudumia.
Sambamba na hilo Mkutano huu pia unalenga kuongeza uwezo wa Viongozi
wetu katika kuongoza watu na rasillimali zingine zilizoko kwenye maeneo
yetu ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya pamoja.
Alisisitiza kuwa Mafunzo haya yatajielekeza katika Kuimarisha Sifa
Binafsi za Viongozi kwa sababu Viongozi ndio wanaowasimamia wananchi
katika kiLA Eneo hivyo ni lazima kila kiongozi aweze kujitenegenezea
Sifa binafsi ili akubalike na kuhesimika katika Jamii husika.
“Sifa hizi binafsi tunazozizungumzia ni Ushawishi, Kuaminika, Uadilifu,
Mtenda Haki, Muumini wa Utawala bora na Utawala wa Sheria na zaidi kuwa
mchahapa kazi na awe na weledi wa hali ya juu sasa haya yote
yatafundishwa kupitia mafunzo haya ya namna gani Kiongozi anaweza
Kujijengea Sifa Binafsi katika Jamii tunazoziongoza.
Akitoa Neno la Shukrani kwa niaba ya viongozi walioshiriki katika
Mafunzo haya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti ameshukuru
OR-TAMISEMI na Taasisi ya Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya na zaidi
ameahidi Umakini wa washiriki kwa siku zote za mafunzo.
Mafunzo haya ya awamu ya Nne na ya mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa imegususa Viongozi kutoka
katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
SHARE
No comments:
Post a Comment