Mwandishi Wetu
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umekuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii nchini kwetu.
Hali hii inatokana na umakini wa viongozi wa mfuko huo kutambua umuhimu wa kutenga sehemu ya kila inachopata katika huduma zake na kukirejesha kwa jamii.
Kimsingi hili ni jambo jema kwa sababu linaharakisha maendeleo na wakati huo huo kusaidia kupunguza umaskini ndani ya jamii yetu.
James Mlowe akizungumza katika moja ya mikutano ya LAPF
Ikumbukwe kwamba mfuko unapotoa msaada mathalani wa vifaa vya afya au elimu vinasaidia kuweka mazingira bora ya utoaji wa huduma za kijamii kwa ufanisi mkubwa.
Ni kwa sababu hii tunahimiza jamii iendelee kujiunga na mfuko huo kwani una fursa mbalimbali, zikiwemo za mikopo kwa ajili ya wanafunzi.
Kwa mfano, mfuko huo ulitoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Tunafahamu shule zetu zinapokosa uzio namna wanafunzi wanavyoishi katika mazingira ambayo si rafiki kupatiwa elimu, lakini LAPF ilipoombwa kuchangia suala hilo haikusita.
Msaada huo utawanufaisha si tu wanafunzi na walimu wa shule hiyo bali wadau wengine ambao wamekuwa wakitumia viwanja vya shule.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Rehema Mkamba (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF kwa Shule ya Sekondari Dodoma.
Ikumbukwe pia kwamba LAPF ni Mfuko wa Pensheni ambao pamoja na mambo mengine jukumu haswa ni kutoa mafao ya pensheni kwa wanachama wake.
Kama hiyo haitoshi, Mfuko wa Pensheni LAPF ulikuwa pia mstari wa mbele katika kuchangia ujenzi wa madarasa wilayani Geita ikiwa jitihada za mfuko kuunga mkono jitihada za Serikali kutoa elimu bure.
Mfuko huo ulitoa mabati 300 yenye thamani ya sh. 7,000,000. Mafanikio hayo yanatokana na uimara wa viongozi wake, wakiwemo Mkurugenzi Mkuu wake, Eliudi Sanga na wengine.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko huo, James Mlowe amekuwa kiungo muhimu katika kufanikisha masuala mbalimbali ikiwemo kuhakikisha taarifa zinazohusu mfuko zinawafikia wananchi.
Si hivyo tu kwani amekuwa daraja pia la kuunganisha mfuko na wadau mbalimbali ili kutambulisha shughuli zake, ndiyo maana mfuko umekuwa ukifanya vizuri na kujipatia tuzo mbalimbali kama ilivyojionesha mwaka jana wakati wa Maonesho ya Sabasaba.
SHARE
No comments:
Post a Comment