Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba
baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la
Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika
mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji
wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa
Idara ya Uhamiaji.

Wafanyakazi na uongozi wa Jeshi la
Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada ya makabidhiano ya
nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye
mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu
Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo
limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji
wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa
Idara ya Uhamiaji.
Mradi huu ambao ujenzi wake ulianza
Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji
uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji
na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63 ambazo zimeshakamilika na
kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara ya Uhamiaji.
Makabidhiano haya yamefanywa na Meneja
Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Itandula Gambalagi kwa niaba
ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa
niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Makabidhiano haya yanafanyika baada ya
ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya
kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.Katika uzinduzi wa nyumba
hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais kwamba nyumba hizi
zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.
Leo ni siku ya furaha kuona kwamba NHC
inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa
nyumba katika mradi huu.Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi
mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira
yake.
Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.
SHARE
No comments:
Post a Comment